MWANAMKE mmoja ambaye  katika maisha yake hakuwahi kufikiria kwenda likizo eneo analolipenda na kuishia kupachika picha yake iliyotengenezwa ndani ya picha za watu waliopo mapumziko, nyota yake imewaka.
Mwanamke huyo Sevelyn Gat ambaye picha zake zimeleta gumzo kubwa katika mitandoa ya kijamii kwa namna ambavyo anazipachika na kuziandikia maelezo ameonwa na mfanyabiashara.
Mfanyabiashara huyo wa Nairobi Sam Gishuru amewezesha binti huyo angalau kwenda likizo nje na kutimiza ndoto yake.
Katika picha zilizokuwa zikitamba katika Facebook page mdada huyo alikuwa anaonekana yupo katika ziara katika maeneo maarufu duniani na kutengeneza ‘gumzo’ kwamba ana furahia eneo hilo alilofika..
Picha zake amezitumbukiza katika picha za watu waliopo kwenye Ukuta mkuu wa China na katika hekali.
Aidha picha nyhingine akiwa na wacheza sinema wa Marekani na Hollywood na kadhalika.
Picha hizo alikuwa anazitengeneza ndani ya dirisha la kutengenezea picha japo katika daraja la chini kabisa kiasi cha kuonekana kupachikwa tu bila uhalisia.
Picha hizo kwa maelezo zimekuwa mgumzo katika mitandao kiasi cha watu  kila anapopachina kujiliza Seve jkwa sasa yupo wapi.
Picha nyingine zinaonesha akiwa nje ya ndege  za kusafiria na kuandika kwamba ameondoka kwenda China kwa mapumziko na nyingine zikionesha ukuta wa China na kusema ni eneo jema na picha nyingine anaonesha kwamba amerejea nyumbani akiwaaga wananchi wa China.
Imeeelezwa na mtandao wa Sick Chirpse, kuwa Sam baada ya kuona picha hizo  aliwakabili marafiki zake kuchangia binti huyo kupata safari ya mapumziko ya kweli, kulala hoteli ya nyota nne, bima na kiasi cha fedha  za matumizi.
Kwa mujibu wa habari binti huyo ataenda kwa ziara ya kitalii ya kweli nchini China.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO