watu wakitoka uwanja wa ndege baada ya mlipuko
WATU 31 wamekufa na wengine 22 kujeruhiwa baada uya kutokea milipuko mfululizo asubuhi ya leo mjini Brussels, Ubelgiji.
Kwa mujibu wa taarifga miwili takaribani miwili ilitikisa uwanja wa ndege wa Brussels wa  Zaventem , huku shirika kubwa la utangazaji la hapa RTBF ikisema kwamba watu 21 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa.
Baadae NBC News ilisema kwamba watu 31 waliuawa 22 wakiwa kituoni na 11 katika uwanja wa ndege.
Imeelezwa kuw amlipko wa uwanja wa ndege ulifanywa kwa njia ya kujitoa mhanga.
Muda mfupi baada ya mlipuiko uwanja wa ndege mlipuko mwingine ulitokea katika kituo cha treni za chini katika viunga vya mji wa Maalbeek karibu kabisa na eneo la Umoja wa Ulaya.
Kutokana na shambulio hilo vituo vyote vya treni za chini vimefungwa na polisiw ameshauri wageni wote kubaki ndani ya makazi yao.
Watu wlaioshuhudia kadhia hiyo wamesema kwamba wameona watu wengiw akiondolewa kwa kutumia vitanda vya wagonjwa kutoka katika uwanja wa ndege.
 Kutokana na mashambulio hayo Ubelgiji imepandisha kiwango cha hali ya hatari kutokana na ugaidi kufikia 4 ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi katika miaka ya karibuni huku ikiaminika kwamba shambulio hilo linatokana na kukamatwa kwa mtuhumiwa ugaidi wa Ufaransa aliyekuwa anasakwa kwa udi na uvumba, Salah Abdeslam.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO