Afisa mkuu wa biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty
KAMPUNI ya simu ya  Airtel Tanzania, kwa kushirikiana na Facebook, imezindua huduma ya  Bure  ya Facebook kwa wateja wa Airtel katika kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la  "Bila Salio Wala MB".
Lengo la mpango huu ni kuunganisha kila Mtanzania katika intaneti  na, kwa njia hii, kuwezesha kufungua fursa nyingi ambazo hapo awali zimekuwa ngumu kwao kuzitimiza. 
Kama sehemu ya "Bila Salio Wala MB" kampeni, Watanzania wenye kadi ya simu ya Airtel na simu yenye uwezo wa kupokea intaneti wataweza kufurahia Facebook, Messenger na huduma nyingine zinazopatikana kwenye facebook. 
Ndani ya Facebook, wateja wataweza kuchat, kutuma picha, video , kutoa maoni, kuweka picha, kuangalia picha na mambo mengine mengi. 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa mkuu wa biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty alisema: "kutokana na maisha ya sasa jinsi yalivyo intaneti ni kitu muhimu sana katika maisha ya watu kwani imekuwa ikileta maendeleo katika Jamii na uchumi duniani kote. Tunaamini kabisa huduma hizi za bure za facebook ni hatua ya kwanza nzuri ya kufikia lengo hili. "
Pamoja na huduma hiyo watapata huduma ya Free Basics ambayo ni seti ya Kiswahili  na tovuti ya kimataifa Tanzania inayotoa Habari za  afya, elimu, biashara na habari za  fedha husiana na watu ili waweze kufanya uamuzi na maamuzi ya kuboresha maisha yao. 
 Free Basics   ni maarufu sana katika mitandao ya kijamii duniani kote , inayowawezesha wateja kuwasiliana kwa urahisi na ndugu jamaa na marafiki zao.
Akitoa maelezo, mkuu wa kitengo cha intaneti Gaurav Dhingra alielezea kuwa utumiaji wa programu hiyo ni rahisi popote ulipo Tanzania, ilimradi unakadi ya simu ya Airtel iliyosajiliwa  katika simu yako yenye uwezo wa kupata intaneti.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO