Msajili wa Hazina Bwana Lawrence Mafuru, akionyesha cheti cha makubaliano ya umiliki wa hisa asilimia 35 za  Bharti Airtel walizokuwa wakimiliki ndani ya  TTCL kwenda serikalini mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel bwana Christian De Faria (kulia) kusaini makubaliano hayo leo.
Serikali ya Tanzania, Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Bharti Airtel Leo wametiliana saini  makubaliano ambapo airtel Bharti itaachia hisa zao 35% walizokuwa wakimiliki katika kampuni ya mawasiliano nchini Tanzania TTCL ili serikali iweze kumiliki kampuni hiyo ya TTCL kwa asilimia 100.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel Afrika Bwana Christian Manuel De Faria “Bharti Airtel tunaishukuru sana serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri tuliokuwa nao kwa miaka mingi kapitia shirika la Tanzania Telecomunication Company Limited (TTCL). 
Bharti Airtel tunatambua mikakati na nia ya serikali kutaka kuwa mmiliki pekee katika shirika la TTCL. kutokana na utaratibu na jitihada zenye maamuzi ya busara toka pande zote Bharti Airtel na Serikali swala hili limefikia tamati. 
Hivyo kwa kumalizika vyema kwa swala hili la kuirudishia serikali hisa 35% zilizokuwa zinamilikiwa na  Bharti Airtel  ndani ya TTCL,  Bharti Airtel tunawakikishia watanzania kwa ujumla kuwa tutaendelea na mikakati bora ya uwekezaji kati yetu na serikali kupitia Airtel Tanzania ambapo Bharti Airtel ni mmiliki wa hisa 60%”. alimaliza kusema De Faria

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO