Chama cha Karate club of Jundokan So Honbu System Tanzania kimepata usajili.

Kutokana na usajili huo Tanzania isasa tasonga mbele na kushika nafasi za kimataifa baada ya usajili huo .

Naye Mkufunzi mkuu au Chief instructor wa chama hicho anayetambuliwa kimataifa na baraza la dunia la karate lenye makao yake Okinawa Japan Sensei Rumadha Fundi, mwenye uzoefu wa vyama vitatu vya Goju Ryu tofauti,  alithibitisha kusajiliwa kwa chama hicho.

Alisema kutokana na usajili huo uliowezesha kwa msaada  mkubwa na watu walio karibu sana nae  amepata nguvu kubwa ya kuiwezesha Tanzania kuwa na mfumo huo wenye asili ya visiwa vya Okinawa, Japan.
Jundokan So Honbu, ni mfumo unaofundisha mtindo wa Okinawa Goju Ryu kwa kuzingatia utamaduni uliowekwa na Master Chojun Miyagi na kusambazwa na mwanafunzi wake ambaye ndiye mwanzilishi wa JUNDOKAN, Master Eiichi Miyazato 1957, huko Asato, Nana, kisiwani Okinawa, Japan.

Jundokan katika Kiswahili sisisi inamaananisha ni  " Sehemu ya mafundisho ya mwanzilishi"JUN +DO+ KAN, "jun"ni imechuliwa toka jina la mwanzilishi wa Goju Ryu, Chojun  na "Do" ikimaanisha mwenendo, " Kan" ikimaanisha shule au mafunzo.

Mfumo huo haujabadilishwa tangu ulipoasisiwa na Master Miyagi.
 
Sensei Rumadha Fundi amesimama mbele ya kumbukumbu ya mnara wa Master Kanryo Higaonna( Mwalimu wa master Miyagi),

Sensei Rumadha Fundi, wakiwa na Sensei Pedro Cardeira toka Lisbon, Ureno wakifanya zoezi la mbinu ya kuvunja mkono,Rumadha amesema mipango ipo njiani ya kuwa na tawi lenye lengo na nia kufuata sheria na kanuni za mfumo asilia tu, bila kubadilisha mbinu  "Kata" kama jinsi inavyo bainika katika mbinu za " Sports Karate" kwenye  uchezaji wa "kata" wa kiujumla.

Hivi karibuni, huko visiwani Okinawa katika makao makuu ya tawi hilo, jumuiya ya sanaa ya mapambano " Okinawan BUDOKAN & Karate Federation", imeitambua "Jundokan So Honbu" kama moja ya mitindo asili"Original" kutoka Okinawa inayozingatia maadili na mafunzo yaliyo achwa na mua sisi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu.

Ufunguzi rasmi wa shule ya karate na uteuzi wa wanafunzi wa kuu wasaidizi ambao Sensei Rumadha atajitoa muhanga kuwasaidia kimbinu na ubora utatangazwa baadae.

Wanafunzi hawa baadae wanatakiwa kuwa umahili na mtindo huu na kuhakikisha wanapata fursa ya kuwa walimu ( sensei) na kusambaza JUNDOKAN SO HONBU Tanzania yote.

"Msingi tunao mzuri na imara kwa wengi wataojumuika nami kuendeleza hii sanaa hapa nyumbani Tanzania", alisema Sensei Rumadha mwenye uzoefu wa mafunzo hayo ya karate zaidi ya miaka 37 chini ya " ma-sensei" wakuu toka pande zote za  dunia, hasa Okinawa, Japan.
SOURCE: Zainab Ally Khamis
Dar es salaam School of Journalism(DSJ)

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO