KIONGOZI  wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis  ameitaka taasisi yake ya elimu Scholas Occurrentes kurejesha fedha kiasi cha peso 16,666,000  sawa na dola za Marekani milioni 1.2.
Fedha hizo zimetolewa na Raius wa Argentina Mauricio Macri.
Imeelezwa kuwa japo wawili hao hawan auhusiano mzuri kutokana na namna rais huyo anavyotekeleza sera zake za kiuchumi, papa hakupenda namba zinazofanya fedha hizo.
Katika maagizo yake kwa taasisi hiyo yenye makao makuu yake nchini Argentina, Papa alisema kwamba haipendi namba 666.
Katioka Biblia namba 666 imeelezwa kuwa ni namba ya shetani au kwa kiingereza "number of the beast".
Imeelezwa kuwa taasisi hiyo imemsikiliza Papa na imerejesha fedha hizo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO