SHIRIKA la Utangazaji la Uingereza , BBC,limesema kwamba  waingereza wamekubali kujiondoa katika Umoja wa Ulaya  (EU) baada ya miaka 43 ya ushirikiano kwa asilimia 52 za kura kwa 48.
Katika taarifa yao ya ubashiri iliyotolewa leo, shirika hilo maarufu la utangazaji duniani limesema kwamba London na Scotland walipiga kura kwa kishindo kubaki katika Umoja huo lakini kura zao ziliathiriwa na muitikio mbovu wa wapiga kura kaskazini mwa England.
Wapiga kura wa  Wales na English waliunga mkono kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja huo.
Wakati hali  inatabiriwa kuwa hivyo na BBC, sarafu ya nchi hiyo dhidi ya dola ya Marekani  imeporomoka kufikia kiwango cha chini ambacho hakijawahi kutokea kutoka mwaka 1985.
Imeelezwa kuwa watu wengi walijitokeza katika kura hiyo ya maoni kuliko katika uchaguzi mkuu mwaka jana.
Waziri kivuli wa fedha wa Labour, John McDonnell amesema upo Umuhimu wa Benkikuu ya Uingereza ( Bank of England) kuingilia kati mseleleko huo ambao ulitokea mara tu baada ya matokeo ya awali ya kujitoa EU kupatikana kutoka Sunderland.
Kiongozi wa UKIP , Nigel Farage  ambaye kwa miaka 20 amekuwa akifanya kampeni ya Uingereza kujitoa EU amesema kwamba matokeo hayo yatakuwa ni ushindi kwa watu wa kawaida na wale  wanyofu wa taifa hilo.
Bw. Farage –ambaye alibashiri watuw anaotaka kubaki Eu kushinda baada ya kura kuonesha kwamba ndivyo itakavyokuwa, amesema kuwa Alhamisi Juni 23 itaingiua katika historia kama siku yao ya uhuru.
Alitoa wito kwa Waziri Mkuu David Cameron, aliyeitisha kura hizo huku akifanya kampeni wananchi wakubali kubaki EU, kuachia ngazi mara moja.
Naye mtu mmoja  kutoka chama cha Labour  amesema kama watu watapiga kura ya kujiondoa ipo haja kwa waziri mkuu kujitathmini mwenyewe katika kiti alichokalia sasa.
Hata hivyo Conservatives wanaounga mkono kujiondoa kwa Uingereza katika EU wakiwamo Boris Johnson  na Michael Gove wametia saini barua inayomtaka waziri mkuu huyo kubaki madarakani hata kama matokeo yatasema waondoke.
Waziri wa zamani wa Ulaya wa serikali ya Labour, Keith Vaz aliiambia BBC kwamba wananchi wa Uingereza wamepiga kura kwa mihemko na kudharau mawazo ya wataalamu ambaow ameonya kuporomoka kwa uchumi wa UIngereza kama watajiondoa EU.
Alisema kwamba uamuzi huo  una madhara makubwa kwa Uingereza, Ulaya na duniani korte.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO