Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Zanlink Sanjay Raja (Kulia), akibadilishana hati ya makubaliano ya udhamini wa ufunguzi na ufungaji wa tamasha la 19 la ZIFF na mratibu wa jukwaa la watoto na vijana ZIFF Robert Manondolo baada ya kusaini mkataba huo, kushoto Zuhira Khaldin Diarra wa Marekani  ambaye anafanya shughhuli za masoko za ZIFF na meneja masoko wa Zanlink Winnie Rongoma (picha na abdallah masangu)

KAMPUNI ya mawasiliano ya Zanzibar, Zee Communications Limited (Zan Link) imeingia mkataba na Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) la kudhamini ufunguzi na ufungaji wa tamasha hilo.

Ingawa haikuelezwa kiasi cha udhamini huo, hii itakuwa maradufu ya udhamini wa kawaida ambao ulikuwa unafanywa na kampuni hiyo kwa miaka takribani 15 sasa.

Tamasha hilo limeingia mwaka wake wa 19.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mkataba huo jana majira ya Magharibi, Mkurugenzi wa Zanlink Sanjay Raja amesema kwamba ushiriki wao unaonesha kutambua umuhimu wa tamasha hilo ambalo  ni moja ya vivutio vya utalii Visiwani humo.

Alisema kwamba  wamekuwa wakidhamini tamasha hilo kwa miaka 15 lakini safari hii wametoa nafasi kubwa ya udhamini kw alengo la kulifanikisha.

Utiaji saini huo ambao umefanyika juzi majira ya magharibi ni sehemu ya kamepni kubwa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa ZIFF , Profesa Martin Mhando wa kulifanya tamasha hilo kudhaminiwa na makamapuni ya hapa nchini kwa lengo la kuendeleza uwapo wake na kulipa heshima ya kitaifa zaidi na umiliki wake.

Kwa miaka mingi tamasha hilo limekuw alikidhaminiwa na makampuni ya kugeni na mashirika ya umoja wa Mataifa.

Mratibu wa Jukwaa la watoto na Vijana ZIFF Robert Manondolo ambaye ndiye alikuwapo kuweka saini kwa niaba ya ZIFF alishukuru kampuni hiyo ya nyumbani kwa udhamini wake na kusema unaonesha namna gani uhusiano wa ZanLink na ZIFF unazidi kukua.

Amesema udhamini wa safari hii si wa kawaida na hivyo kuleta hali mpya katika uendeshaji wa tamasha hilo ambalo huingiza wageni lukuki kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Hata hivyo aliwataka watanzania kuendelea kulidhamini tamasha hilo ili liweze kuendelea kutimiza malengo yake ya kukuza utamaduni wa filamu na  kuwa pia eneo la uwekezaji na uuzaji wa filamu za kwetu na za kigeni.

Tamasha hilo la filamu kubwa Afrika Mashariki na Kati linatarajiwa kufunguliwa Julai 9 na kuendelea hadi 17 na litaonesha filamu za ndani na nje takribani mia moja na kuendesha majukwaa ya watoto na wanawake, tamasha ndani ya tamasha ambapo filamu kutoka matamasha mengine rafiki huoneshwa, muziki na makongamano  yanayohusu utaalamu wa utengenezaji wa sinema.

Mwisho


Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Zanlink Sanjay Raja (Kulia), wakipongezana huku wakibadilishana hati ya makubaliano ya udhamini wa ufunguzi na ufungaji wa tamasha la 19 la ZIFF na mratibu wa jukwaa la watoto na vijana ZIFF Robert Manondolo baada ya kusaini mkataba huo juzi. Kushoto ni  Meneja masoko wa ZIFF, Zuhira Khaldin Diarra.(Na Mpigapicha wetu)

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO