Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dk. Abdallah Posi amewataka wadau wa huduma za kifedha vijijini kuhakikisha kwamba huduma yao hiyo inakuwa shirikishi na kujali makundi maalumu ili kuyatoa katika umaskini.
Dk Posi alisema hayo hivi karibuni wakati akifungua mkutano wa Mwaka wa Shirikisho la Taasisi na Asasi za Fedha Nchini (TAMFI) ambao pia unajadili  suala la ushirikishaji wa wananchi vijiji katika sekta ndogo ya fedha ili kuinua uchumi wao.
Alisema kwa kuwa wananchi wengi wapo vijijini uwapo wa huduma za kifedha kwao zinazozingatia ushirikishaji kutabadili maisha ya vijijini na kutanua wigo wa fursa.
Naibu waziri huyo alisema kwamba kwa sas amabenki si rafiki wa wananchi na kwamba kuwapo kwa huduma zinazomlenga mwananchi wa kijijini kw akutumia taasisi za kifedha kutasaidia kubadili mitazamo.
Alisema makundi maalumu kama wanawake na walemavu wamekuwa wakiachwa nyuma katika huduma za kifedha na kutaka mkutano huo kujadili kwa kina namna ya kuwawezesha wananchi wa vijijini kubadili maisha kwa kuwa na uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo kwa kuzingatia shughhuli za kilimo, ufugaji na uvuvi walizonazo.
Alisema watu wote ni sawa na kwa kuwa mkutano unajadili jambo jema ni vyema wakaangalia masuala ya mila na utamaduni yanavyoathiri huduma za fedha na hasa makabila yanayohama maeneo yao kwa sababu za mfumo wa maisha kama wafugaji.
Alisema mambo matano yatayoangaliwa katika mkutano huo yawezeshe kupeleka na kuimarisha huduma za fedha vijijini ambayo itawakuwa rafiki.
Mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo wa siku mbili ni pamoja na  mazingira ya kisheria na kanuni yanayoruhusu ushindani na kumlinda mteja, teknolojia inavyoweza kusaidia kupeleka huduma vijijini, utoaji wa huduma inayomlenga mtu wa kijijini, haja ya kufadhili kilimo,ufugaji na uvuvi na mfumo utakaowezesha kasi ya utoaji wa huduma ya fedha vijijini.
Aidha Naibu waziri huyo alitaka makampuni yanayosaidia makundi maalumu kuhakikisha kwamba misaada yao hiyo inawafanya wapokeaji kuwa wadau wao kwa kuwa itawatoa katika umaskini unaowafanya wawe tegemezi.
Aidha alitaka mkutano huo kuzungumzia kukuza mitaji  ili kupunguza kundi la wategemezi.”Huduma za kibenki si rafiki kwa wananchi wetu wa vijijini, hivyo tunapowawezesha kwa kuwa tumewalenga na tumewashirikisha tutawapatia mitaji ambayo itawafanya kuinuka kiuchumi” alisema Dk Posi ambaye alisisitiza katika hilo usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa kila kundi kuwa kitu cha kwanza kuangaliwa.
 Mkutano huo ulioandaliwa na TAMFI kw akushirikiana na  MIVARAF na Ofisi ya waziri Mkuu   utajadili mada tano na kutoka na tamko la kufanyia kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao.
mwishoPost a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO