Askari Polisi wakiwa na gari kubwa maalumu linalotumika katika  kukabiliana na uvunjifu wa amani wakishiriki kuzima  moto  sehemu ya jengo ya kiwanda cha Nguo cha 21st Century Textiles (1998) Ltd, zamani  kikijulikana kwa jina la  ‘ Polytex’  kilichopo eneo la viwanda Kihonda , Manispaa ya Morogoro. Moto huo ulizuka majira ya saa 12 asubuhi  leo.


Tingatinga la kiwanda  cha 21st Century Textiles ( 1998)Ltd, zamani  kilichokuwa kikijulikana kwa jina la ‘Polytex’ kilichopo eneo la viwanda Kihonda , Manispaa ya Morogoro,likivunja  sehemu ya ukuta kwa ajili ya kutoa nafasi ya kuwezeshwa askari wa kikosi cha zimamoto na Polisi kuzima  moto  ambao ulitokea majira ya saa 12 asubuhi ya Julai 19, mwaka huu  eneo la ufumaji wa nguo la kiwanda hicho.

Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda  cha 21st Century Textiles( 1998) Ltd , zamani  kikijulikana kwa jina la ‘ Polytex’ kilichopo eneo la viwanda Kihonda , Manispaa ya Morogoro,wakisukuma rotoba la pamba kutoka ndani ya eneo la ufumaji wa nguo  mara baada ya kutokea moto  majira ya saa 12 asubuhi ya Julai 19, mwaka huu.( Picha zote na mdau Nditi).


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO