MAKAHABA wa Nigeria chini ya mwavuli wa Ohotu Diamond Women Initiative, wamewashutumu polisi kwa kuwanyanyasa kama vile wao si binadamu.

Makahaba hao wamesema kwamba wamekuwa wakivamiwa na polisi ambao pamoja na kuwanyanyasa wamekuwa wakiwabaka bila hata kutumia kinga.

Wanawake hao wamesema kwamba wanataka kutambuliwa wao kama binadamu na kutendewa vyema na kwa heshima.

Wamewataka polisi kuwa waungwana .

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya  SafeHeaven Development Initiative, Magaret Onah anasema polisiw anatakiwa kuwakamata makahaba kama watu wengine na kuwafikisha mahakamani lakini si kw anamna wanavyowafanya wakiwafanya wao kama si binadamu hata chembe.

Amesema kitendo chao wao kuwabaka bila kinga  ni kitendo cha udhalilishaji kinachofanywa na jeshi hilo ambalo kazi yake ni kulinda amani  na mali za wananchi.


Aidha makahaba hao wametaka kutambuliwa kwa huduma yao wanayoitoa kwa jamii na kusema kutyotambuliwa kwao ndio kunawafanya polisi kutengeneza kiburi cha kuwanyanyasa na kuwatendea mambo mabaya.

Taarifa ya mamalamiko hayo ya makahaba  yametolewa kupitia mtandao wao wa  Ohotu Diamond Women Initiative (ODWI),  na kutaka mamlaka husika ziwasaidie kuondokana na manyanyaso hayo.

Katika taarifa yao wamesema kwamba sasa wamekuwa viumbe waishio katika hatari ya kutoweka kwa kugeuzwa dango na polisi kila mara.
 Walisema polisi wamekuwa kila mara wakiwavamia katika maeneo yao ya kazi, kuwanyanyasa na kuwabaka bila hata kutumia kinga (kondomu).

“ Wahudumu wa ngono (waliwazaji-makahaba) wanahitaji kuheshimiwa na kuthaminiwa haki zao za msingi za kulindwa dhidi ya manyanyaso ambayo kila serikali inatakiw akufanya kwa wananchi wake.Katika matukio mengi ambapo polisi wanawanyanyasa wahudumu wa ngono, hakuna hatua zinachukuliwa  dhidi yao” inasema taarifa hiyo.

Wamesema kwamba wahudumu hao wa ngono pamoja na huduma yao wamekuwa hawathaminiwi wala kulindwa na sheria wakati wanaponyanyaswa na polisi, wateja na pia jamii inayowazunguka.

 “Kuna ubaguzi  mbaya kabisa kwa wahudumu wa ngono. Tunataka manyanyaso haya yakome mara moja na wanaofanya hivyo wachukuliwe hatua. “

Wamesema mara kwa mara polisi wanavamia makazi yao wanavunja milango na kuwasomba kuwapeleka stesheni za polisi ndani ya magariw akiwa wamewajaza kama mbuzi.

Wanasema kama makahaba hao hawana fedha za kujidhamini wao wenyuewe , polisi watawaambvia wanataka kungonoana nao bila kondomu ili wawaachie, jambo ambalo wamesema ni la kuwanyanyasa.

 “Kama makahaba katika madanguro yetu tunatumia kondomu lakini polisi wanapokukamata wanakulazimisha kufanya mapenzi nao bila kinga, hii ni mbaya kabisa,” taarifa hiyo imesema.

Ripoti hiyo pia imemkariri Mkurugenzi mtendaji  wa SafeHeaven Development Initiative  Magaret Onah, akisema kitendo cha polisi kuvamia madanguro na kuwabaka watoa huduma hiyo ya ngono ni unyanyasaji wa hali ya juu na kutaka wahusika wachukuliwe hatua kali
“Ni vyema kama wafanyakazi hawa waliwazaji wakapelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka lakini si kwa kuwanyanyasa, kuwachukulia fedha zao na mali zao kwa nguvu na kuwabaka bila kinga. “ alisema Onah.

Alitaka Polisi kubadili namna ya kufanya shughuli zao , hata kama ukahaba ni kinyume cha sheria , kwani hawawezi kuamua kumuua kila mtu anayefanya ukahaba.

 “Wahudumu wa ngono ni raia wan chi hii, ni lazima waheshimike kama raia wengine,”  alisema.

Wafanyakazi hawa wa tasnia ya kuliwaza wanasema kwamba si polisi tu wanaowashughulikia vibaya bali wakati wmingine wateja wanawafanyia kufuru.

Source: https://www.naij.com

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO