Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata akizungumza na waandishi habari juu zuio la taasisi za fedha na kampuni za simu kukata  miamala ya kodi ya ongezeko la thamani VAT leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kamishina wa Mapato ya Ndani wa TRA,  Elijah Mwandumbya.

SERIKALI  imezuia taasisi za  fedha  hasa benki pamoja na kampuni za simu za mkononi kutoza ongezeko la thamani (VAT ) kwa walaji (wananchi).

Akizungumza jana na waandishi habari  jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Alphayo Kidata amesema kuwa fedha ambayo walikuwa wanakata haina ongezeko la thamani hivyo taasisi za fedha (Benki) kampuni za simu zimetakiwa zisiongeze miamala kwa wateja kwa kizingizio cha ongezeko la thamani.

Amesema kuwa fedha iliyokuwa ikikatwa imekuwa haikatwi hivyo kwa sheria hiyo inataka miamala  hiyo iliyokuwa ikikatwa ikatwe asilimia 18 ya thamani ya ongezeko.

Aidha amesema TRA haijaweka muongozo wa juu ongezeko hilo kwa taasisi fedha na kampuni za simu hivyo kwa watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua.

Kidata amesema kuwa wananchi wametakiwa wasiguswe kabisa katika ongezeko hilo kutokana na kutohusika na kufanya hivyo ni makosa.
Source:  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO