MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 6 Julai 2016. Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli kwa nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-

 (a)                Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote yaani Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepanda ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 1 Juni 2016. Kwa Mwezi Julai 2016, bei za rejareja zimepanda kama ifuatavyo; Petroli Sh 23/lita sawa na asilimia 1.26, Dizeli
Sh88/lita sawa na asilimia 5.36 na Mafuta ya Taa Sh 80/lita, sawa na asilimia 5.01, sawia. Aidha, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita bei za jumla nazo pia zimepanda   kama ifuatavyo; Petroli Sh 23.46/lita sawa na asilimia 1.34,   Dizeli Sh 87.54/lita sawa na asilimia 5.74 na Mafuta ya Taa Sh80.48lita sawa na asilimia 5.37, sawia. Kwa kiasi kikubwa, mabadiliko haya  ya bei za mafuta katika soko letu la ndani yametokana na kuendelea kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia. 

 (b)               Mamlaka inapenda kuujulisha umma  kwamba bei kikomo za mafuta kwa eneo husika, zinapatikana vile vile kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

 
(c)                Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

 
(d)               Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo ziwe chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapishwa katika Gazeti la Serikali Na. 70/2016 la Mwezi  Februari 2016. (e)                Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili
kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

 
(f)                Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo;

 Dar es Salaam Petrol 1,888; Dizel 1,720;Taa 1,687

 Katika hatua nyingine Ewura imeonya wafanyabiashara wanaosuasua kununua mafuta kwenye maghala wakisubiri mabadiliko ya bei kwani watachukuliwa hatua kali! 
 
Hadi jana tarehe 4, mafuta ya petroli yakiyouzwa kwenye maghala ili kuwa lita 3,663,950 wakati matumizi kwa siku ikiwa ni lita 2,800,000!
 Huku dizeli iliuzwa 5,532,000 wakati matumizi kwa siku ikiwa ni lita 4,900,000! Hiyo inaonesha hali ya mafuta hapa nchini ni nzuri.

 Titus Kaguo 
Manager-Communications & PR
EWURA
+255759242450
+255713242450
+255786444944
Sent from my iPhone

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO