SHAMBULIO la bomu katika hospitali ya Quetta nchini Pakistan limeua watu 53 na wengine kujeruhiwa.
Shambulio hilo limefanyika katika lango kuu la idara ya dharura.
Imeelezwa kuwa shambulio limefanyika wakati mwili wa mwanasheria mahsuhuri nchini humo ulipokuwa unaingizwa kwa ajili ya hifadhi. Baada ya kuuawa mapema leo.
Imeelezwa kuwa watu walikumbwa na dhoruba hiyo kikamilifu ni waandishi wa habari na wanasheria walioambatana na  mwili wa mwanasheria huyo Bilal Anwar Kasi.
Aidha baada ya shambulio hilo la bomu milio ya risasi ilisikika. Haijajulikana nani anahusika na mashambulio hayo.
Polisi wa Pakistan wamesema kwamba wanaamini kuwa shambulio hilo limefanyw ana mtu wa kujitoa mhanga.
Kasi aliuawa wakati akielekea mahakamani mjini Quetta

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO