BINADAMU anayemainika kuwa na kasi zaidi katika karne ya sasa Usain Bolt (29) amefanya mkutano na waandishi wa habari ambao ulikuwa na raha ya aina yake jinsi ilivyopangiliwa kabla ya kuingia katika patashika ya Olimpiki.
Waandishi wa waliokuwapo katika mkutano huo hawakuboreka jinsi jamaa alivyochechua.
Usain Bolt anmbaye alizungumza na waandishi wa habari Jumatatu wiki hii pamoja na kuthibitisha kwamba hii itakuwa olimpiki yake ya mwisho alisindikizwa na wacheza samba waliotia nakshi ya hali ya juu ambapo Bolt pia alicheza nao kama zinavyoonesha.

Mkutano huo na waandishi wa habari uliandaliwa na  Shirikisho la Olimpiki la jamaica na kampuni ya Puma.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari nchini hapa, Bolt aliulizwa kama ana uhakika wa kushindana na wapinzani safi, ambao hawatumii dawa hizo, alijibu: "Katika maisha hakuna kitu chenye uhakika.”
"Kwangu kwenda kushinda sina wasiwasi na hilo. Nitakwenda na kushindana.
"Naweza kusema kuwa nafikiri tunakwenda katika mwelekeo sahihi. Nafikiri tumewaondoa wale wabaya. Tunatakiwa kupita katika hali mbaya kabla hatujafika katika kipindi kizuri.”
atika mkutano huo pia Usain Bolt anakiri kuwa hana uhakika kama atatetea mataji yake ya Olimpiki .hata hivyo Mwanariadha huyo amesema ana nia ya kukamilisha medali‘tatu’za dhahabu na anakwenda katika michezo hiyo ya Olimpiki akiwa anashikilia ubingwa wa meta 100, 200 na zile za kupokezana vijiti za 4x100.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO