Bi Shakila  Said mwanamuziki mkongwe wa taarab amefariki ghafla baada ya kumaliza kuswali nyumbani kwake Mbagala Charambe wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam.
 Ameanguka ghafla alikua haumwi.. Marehemu atakumbukwa kwa wimbo maarufu usemao  nikimkumbuka wangu maridhiya... Macho yanalia moyo unacheka... ..
Taarifa ya kifo hicho ililetwa katika blogu hii na Addo November rais wa  shirikisho la muziki tanzania  na ametaka wapenzi  na wanamuziki kuwasiliana naye  kwa 0754396367  kujua mambo mbalimbali ya msiba huo.
Taarifa zilizopatikana baadae zinasema kwamba marehemu atazikwa leo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO