pilipili manga zikiwa shinani

Bei ya pilipili manga wilayani Muheza imepanda mara dufu kutoka sh. 4,000 hadi 24,000 kwa kilo mwaka huu baada ya kufanikiwa kuwadhibii wanavijiji wenzao waliokuwa wakijihusisha na uuzaji wa zao hilo kabla ya kukomaa.

Imeelezwa kuwa wakulima kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri walijiwekea sheria ndogo za kudhibiti uvunaji holela wa pilipilimanga  ngazi ya vijiji.

Afisa Kilimo wa kata ya Tongwe, Subira Mmbago alisema baadhi ya wakulima wenye tamaa ya kupata fedha za haraka kwa kushirikiana na wafanyabishara kwa makusudi waliamua kuharibu soko la zao hilo kwa kuvuna Pilipili Manga kabla ya muda wake wa kukomaa na kisha kuivumbika (Kuipepea)ndani ya chombo chenye maji yaliyochemshwa (ya moto) ili kutengeneza rangi nyeusi sawa na rangi halisi ya Pilipilimanga iliyokomaa.

“Kitendo hicho cha kupepea Pilipilimanga kwa maji ya moto ili  kubadilisha rangi ya pilipilimanga changa ili ionekane  kama imekomaa  kwa kiasi kikubwa kiliwaudhi sana wanunuzi wa zao hilo hasa waliokuwa wakitoka nje ya nchi kwasababu bei sokoni ililazimika kushuka hadi kufikia sh. 4,000 kwa kilo tofauti na ilivyokuwa awali katika miaka mitatu iliyopita,”alisema na kuongeza.

 
zinavyoonekana mara tu baada ya kuvunwa

Zikianikwa ili kukauka kabla ya kuzifikisha sokoni

“Madhara ya upepeaji wa pilipilimanga kwa urahisi yaliweza kuonekana siku saba tu baada ya shughuli hiyo kufanyika …. Kwa hiyo wafanyabisha hao wasio waaminifu walikuwa wanategea na hivyo mteja baada ya kununua anajikuta pilipilimanga inaanza kupukutika yenyewe kama unga tofauti na ile ambayo imekomaa mtini kabla ya kuvunwa,”alisema.

Vijiji vinavyolima pilipili manmga wilayani Muheza ni pamoja na  Tongwe, Kisiwani, amani na Magoroto.
Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO