Watu waliokufa katika ajali ya Kondoa ni watatu na wengine 30 wamejeruhiwa.
Watu hao wamekufa kwenye gari walilokuwa wakisafiria kutoka msibani ambalo liligongana na gari linalotengeneza barabara ya Kondoa-Manyara katika eneo la Humai wilayani Kondoa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali, watu hao walikuwa wakitokea kwenye msiba wa ndugu yao aliyekuwa akiishi Palanda wilayani Chemba.
Taarifa zilisema kwamba ajali hiyo ilihusisha gari dogo la abiria aina ya Toyota Coaster namba T567 BAH lilokuwa likiendeshwa na Eliab Juma liligongana na gari namba T269 AZL aina ya Isuzu mali ya kampuni ya wachina ya CRG inayojenga barabara hiyo.Isuzu hiyo ilikuwa ikiendeshw ana dereva aliyetambuliwa kwa jina moja Alfa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa1:30 usiku wa kuamkia jana katika eneo hilo.
 Kamanda Mambosasa aliwataja waliofariki dunia kuwa ni wakazi wa Moshi eneo la Mabogini, Hamida Juma (35), Abubakar Athuman (54) na Samira Amir (32).

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO