Mwanamuziki maarufu  wa miondoko ya Kwaito, Mduduzi Tshabalala al maarufu kama Mandoza amefariki dunia leo asubuhi wakati akikimbizwa hospitalini na mkewe.
Mandoza Mei mwaka jana alibainika kuwa na kansa ya ubongo, ambayo pia katika siku za mwisho ilimtia upofu.
Mwanamuziki huyo ambaye amekufa akiwa na umri wa miaka  38 atakumbukwa kwa vibao vyake vitano maarufu vya Nkalakatha, 50-50 (M'du feat Mandoza), Uzoyithola Kanjani, Sgelekeqe na Godoba.
Tshabalala alianza shughuli za muziki kw akuunda kundi la Kwaito la Chiskop, akiwa na marafiki zake watatu wa wakati wa utoto wake. Ingawa kundi hili lilipata mafanikio makubwa, Mandoza alianza kwenda solo mwaka 1999 wakati alipofyatua albamu yake ya kwanza, 9II5 Zola South.
Albamu hiyo ilifanya vyema sokoni na mwaka 2000 alifyatua nyingine ya Nkalakatha.  Traki ya Nkalakatha imetumika sana katika radio mbalimbali za Afrika Kusini na kumpatia tuzo ya muziki bora wa mwaka katika tamasha la muziki la Afrika Kusini mwaka 2001. Albamu yake hiyo pia ilipata tuzo ya kuwa  na muziki bomba wa kwaito.
Mke wake Mandoza, Mpho alisema kwamba asubuhi mumewe alikuwa anapata shida ya kupumua na kuamua kumkimbiza hospitali lakini kabla hajavuka geti la hospitali, gwiji huyo aliacha dunia.
Mandoza  alipangwa kushiriki katika tamasha la muziki la SABC katika uwanja wa Orlando Septemba 24. 

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO