MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA) imeanza mchakato wa kubaini Kaya maskini zitakazonufaika na mpango wa kupata huduma ya maji bila malipo.
Hatua ya kufanywa mpango huo wa kupata kaya maskini ni utekelezaji wa Sera ya taifa ya Maji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa, Joshua Mgeyekwa amebainisha hayo wakati akifungua semina maalum ya siku moja kwa maafisa Tarafa, baadhi Watendaji na Wenyeviti wa mitaa watakaohusika katika zoezi hilo la utambuzi.
Alisema kupitia mpango huo Tanga Uwasa inakusudia kuongeza idadi ya kaya zinazolipiwa huduma ya majisafi kutoka 28 za sasa hadi kufikia kaya takriban 100 ambazo zitabainika kupitia vigezo vilivyowekwa kwamba kweli hawajiwezi.
Nao baadhi ya washiriki akiwemo Mwenyekiti wa mtaa wa Kombezi, Rashid Sembe aliishukuru mamlaka kwa kutekeleza agizo hilo la serikali.
Afisa Mtendaji Kata ya Maweni, Rehema Said alisema utaratibu wa kutambua watu wasiokua na uwezo  kupitia ngazi za mitaa hadi tarafa utakuwa wa haki bila ya upendeleo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO