Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel,Warren Kanga (kushoto) na Umilkheri Matata wakichuana  katika shindano la kucheza muziki ikiwa ni sehemu ya burudani kusherehekea siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kampuni ya simu ya mkononi ya aAirtel Tanzania yasherehekea siku ya wanafamilia mwishoni mwa wiki hii Kunduchi Wet n Wild .
 Ni muda muafaka kwa familia mbali mbali kuwezakujuana na  kujumuika kwa pamoja na kuweza kubadilishana mawazo na hata kufurahia mafanikia ya matunda waliyoyapata kwa mwa huu.
 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya alisema ni desturi yao kuwa na siku maalumu kila mwaka ya kuwakutanisha wafanyakazi wao na familia zao ili pamoja na kushiriki michezo na mambo mengine ya kuburudisha nyoyo zao zao lakini pia huitumia siku hiyo kuzidi kuimarisha mshikamano miongoni mwao. 
 
Mmoja wa watoto wa  wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, Beatrice Moses akifurahia mchezo wa kuraka ndani ya bwawa la kuogelea katika bonanza la siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

WATOTO wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, wakifurahia ndani ya bwawa la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Afisa Rasilimali wa watu, Mubaraka Kibarabara wa Kampuni ya Simu za Mkononi YA Airtel (kulia), akimpa zawadi Beatrice Nalingigwa baada ya kuibuka kidedea katika shidano la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

"Umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu mahali pa kazi, lakini pia ukiwa na mfanyakazi anayetoka katika familia iliyokosa utulivu, lakini pia mfanyakazi legelege hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi," akaongeza Bwana Foya. 
Zaidi ya wafanyakazi na wanafamilia  600 walishiriki katika bonanza hilo na kushiriki michezo mbalimbali kama vile kucheza muziki,kuvutaka kamba, soka la baharini, wavu na kuogelea. 
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakishindana.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO