WAFANYABIASHARA soko Kuu la Morogoro ambalo lilijengwa mwaka 1953 wameanza kubomoa  maeneo yao kwa hirari  kuanzia leo kupisha ujenzi wa soko jipya lenye ghrofa mbili.
Tayari halmashauri ya manispaa ya Morogoro imeingia mkataba na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) kwa ajili ya kupatiwa mkopo wa fedha zitakazosimamia mradi wa ujenzi wa soko jipya.
Leo wafanyabiashara wengi walikuwa katika hekaheka ya kubomoa kwa hiari yao vibanda vya maduka na  kuhamisha bidhaa zao.

Vibanda vimekuwa vikiondolewaNazo nyaya zimeanza kuondolewa kupisha ujenzi


Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Mgalula amesema kwenye mazungumzo na wandishi wa habari  kuhusiana na uamuzi wa kuvunjwa kwa soko kuu hilo lililojengwa tangu mwaka 1953
Hivyo alisema , kutokana na soko hilo kutokuwa na kesi mahakamani na michoro ya ramani kukamilishwa , kinachofuatiwa ni kumpata mshauri wa kuendesha tathimimi ya kimazingira na kuiwasilisha Benki kwa ajili ya kusaini mkataka wa kupatiwa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa soko jipya na la kisasa.
Ujenzi wa soko jipya unatarajia kuchukua muda wa mwaka mmoja na likakapo kamilika kipaumbele kitawekwa kwa wafayabiashara waliopisha ujenzi
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo  wafanyabiashara wanaotoka hapo wametafutiwa nafasi maeneo ya Nane Nane, Kihonda, Mazimbu, Sabasaba, Mawenzi  na eneo la Mazense na kwa wenye vibanda vya maduka wametakiwa kujitafutia wenyewe maeneo yatakayowafaa  kulingana na makubaliano yaliyopo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO