MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mkinga, mkoa wa Tanga , Emmanuel Mkumbo (41) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa  Morogoro kwa tuhuma za kutishia kumuua kwa  bastola askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa na kuvunja sheria za usalama barabarani.

Mkumbo ambaye ni  mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam , leo alipandishwa kizimbani na kusomewa  mashtaka hayo mbele ya hakimu Agripinas Kimanze , kutoka kwa  Mwendesha mashtaka wa Serikali ,Sunday Hyera, akisaidiana na Ediga Bantulaki.

Kwa mujibu wa waendesha mashitaka hao wa Serikali kuwa,  mtumiwa huyo anakabiliwa na kesi mbili ya kwanza ikiwa ni kesi ya jinai kifungu cha 226 ya mwaka 2016 na ya pili ni kesi ya usalama barabarani kifungu cha 222.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 15, mwaka huu eneo la Mkambarani, wilaya ya Morogoro katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaamm wakati akiendesha gari aina ya Totota Pajero yenye namba za usajili T 845 CTJ .


Kosa la kwanza linalomkabiri Mkurugenzi mtendaji huyo ni  kujaribu kumtishia kumuua kwa bastola askari aliyejulikana kwa jina la Koplo Titunda, akiwa katika majukumu yake ya kikazi  na makosa mengine ni  kuendesha gari lenye namba T845 CTJ aina ya Totota Pajero bila ya kuwa na leseni na kuendesha gari bila  bima.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO