KUMETOKEA hali isiyoeleweka ya vifo vya makahaba watatu wa danguro la Umuahia, jimbo la Abia nchini Nigeria na wateja wao.
Taarifa za mtandao  za Abia Facts Newspaper (AFN) zinasema kwamba watu hao sita walikutwa asubuhi wamekufa katika hoteli inayojulikana kwa jina la 50-50 iliyopo katika jimbo laAbia.
Aidha watu wengine wawili walikutwa hawajitambui.

 

Abia Facts Newspaper (afn) waliendelea kusema kwamba makahaba wazee ambao waliishi katika hoteli hiyo iliyopo mtaa wa Uyo huko Umuahia, walilalamika kwamba walishawagi tandikwa makofi ya nguvu na watu au kitu kisichojulikana.
Katika tukio hilo wiki moja iliyopita makofi hayo yalimpoteza fahamu mwenzao mmoja na hivyo kuamua kuondoka.
Hata hivyo mwenye danguro hilo alijiri makahaba wengine kutoka miji mingine kuendelea na biashara yake.
Lakini makahaba hao wapya watatu na wateja wao wamekutwa wamekufa na hivyo watu kukosa nafasi ya kujua nini kiliwapata.

Polisi wa Nigeria baada ya tukio hilo waliizingira hoteli hiyo kuwezesha usalama kutokana na kundi kubwa la watu kufika kufuatilia taarifa hizo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO