Waziri  wa Nchi Ofisi ya  Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba, ( watatu ) akiongozana na baadhi ya  watendaji Mamkala ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Morooro ( MORUWASA) na wengine kutoka  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),  Mamlaka  ya Bonde la Wami -Ruvu pamoja na Manispaa ya Morogoro  kutoka eneo  la chanzo ya maji cha Mambogo  katika safu ya Milima ya Uluguru jana , ( Okt 16) alioanza ziara ya siku mbili mkoani Morogoro.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya  Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba, ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kushirikiana na Mamlaka  ya Bonde la Wami -Ruvu na Manispaa ya Morogoro kuwaondoa watu  waliojenga makazi katika  chanzo ya maji cha Mambogo  safu ya Milima ya Uluguru ifikapo Novemba mwaka huu.

Hatua hivyo inatokana na uharibifu wa mazingira na uchepushwaji wa maji katika chanzo cha mto huo kwa ajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji na kusababisha kukosekana kwa maji kwenye chanzo chake kutoa ya uzajo mita milioni saba kwa siku na kupungua hadi milioni tatu kwa siku. 
 
Waziri  wa Nchi Ofisi ya  Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba, ( kati kati aliyeweka mikono kufuani ) akijadiliana jambo na watendaji wa  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),  Mamlaka  ya Bonde la Wami -Ruvu pamoja na Manispaa ya Morogoro  eneo la chanzo ya maji cha Mambogo  katika safu ya Milima ya Uluguru jana , ( Okt 16) alioanza ziara ya siku mbili mkoani Morogoro, iwango cha uzajo wa maji kimepungua katika chanzo hicho.


Waziri Makamba baada ya kutembelea chanzo hicho cha Mambogo na kujionea upungufu mkubwa wa maji kutokana na maeneo ya milima ya  chanzo cha mtu hiyo  kuvamiwa na watu kwa kujenga makazi na uchepushaji maji kwa ajili ya shughuli zao za  kilimo cha umwagiliaji  alisema , bila kuchukua hatua hiyo , Serikali itakuwa imepata  hasara kubwa  baada ya kujenga miundombinu ya kisasa ya  matangi makubwa na mitambo ya kuchunja maji ambapo kwa pamoja imegharimu zaidi ya Sh bilioni 15 hadi 16 , fedha za ndani na misaada ya   wahisani.

“ Watu ambao hawajaondoka , waondoke mapema na haraka sana , waambiwe hilo na tupeane muda ni lini waondoke , Novemba mwishoni mwa mwaka huu  wamewaomeondolewa waliojenga kwenye eneo la chanzo hiki” alisema Makamba mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro.

Waziri Makamba , pia Ofisa wa Bonde la Wami – Ruvu, Praxeda Kalungendo ,na watu wake kushirikiana na  maofisa wa NEMC Kanda ya Mashariki ambao wana nguvu za kisheria na halmashauri ya Manispaa hiyo kuendesha  ukaguzi  ili kubaini watu waliochepusha maji.

Waziri aliwataka kuanza kazi hiyo mara moja na wale watakaokutwa wamechepusha maji kwa shughuli zao  wakamatwe na wafikishwe mahakamani kulingana na sheria ya hifadhi ya mazingira .

 Source:  John Nditi, Morogoro


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO