MWANAMUME aliyesema kwamba amefanya ngono na wasichana na wanawake takribani 104 kama sehemu ya kuwaingiza ukubwani na kuwatoa nuksi nchini Malawi  huku akijua kwamba anaishi na virusi vya Ukimwi amepatikana na hatia na hukumu yake itasomwa Novemba 22.
Mtu huyo Eric Aniva alikamatwa na kufikishwa mahakamani baada ya kufanya mazungumzo ya kina na Shirika la Utangazaji la Uingereza kuhusu ufanyaji huo mapenzi wenye lengo la kuondoa nuksi kwa wanawake na pia kuwaingiza ukubwani mabinti.
Mwanamume huyo alikamatwa nyumbani kwake Julai mwaka huu baada ya kukiri kwamba alifanya mapenzi na mabinti ambao wengine walikuwa ni vijana wa miaka 12 huku akijua kwamba anaishi na virusi vya Ukimwi na asiwaambie kitu.
Aniva anasema kwamba alikuwa anakodishwa na ndugu wa mabinti hao kufanya nao ngono kama sehemu ya kuwaingiza ukubwani na wakubwa kuwaondoa nuksi hasa waliofiwa.
Inaaminika kwamba  kama mwanamke aliyefiwa hatafanyiwa matendo hayo anaweza kuandamwa na bahati mbaya, kifo cha ghafla na hata ugonjwa.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO