WATU watano wamekuna sita kujeruhiwa vibaya baada ya kudondokewa na mwamba wa mawe katika (shimo) la mgodi mkubwa wa zamani wa Resolute uliopo wilayani Nzega Mkoani Tabora.
Mkuu wa wilaya ya Nzega  Godfrey Ngupulla akizungumzia tukio hilo alisema limetokea majira ya saa saba mchana Dec 29 mwaka huu baada ya kundi la wachimbaji wadogo wa mgodi wa Umoja kuvamia eneo hilo ambalo limepigwa marufuku na serikali.
Aliwataja walipoteza maisha kuwa ni pamoja na Joseph Mpenda mkazi wa shinyanga,Mohamed  mohamed mkazi wa singida ,Manona Nyombi mkazi wa Bariadi pamoja na na Modesta Leonard mkazi wa Nzega moja hajatambulika .
Aliwataja majeruhi ni Kangwa Mayenga(22) mkazi wa bariadi,Agness Antony(40)   mkazi wa chato, Deus Alphonce(45) Mkazi wa Igunga pamoja na Matias Mapunda mkazi wa chato alisema wote kwa pamoja wanaendelea kupata matibabu ila wawili majina yao hayakupatikana kutokana na majeruhi hao kuwa maututi na hawawezi kuongea.
Wakizingumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wachimbaji waliokuwa wakiokoa miili ya marehemu walisema kuwa sababu ya kuingia katika eneo hilo la serikali ni ukosefu wa maeneo ya kuchimbia.

hata huvyo Mbunge wa jimbo la Nzega mjini Hussein Bashe akiwa katika maeneo hayo alisema tayari hatua za awali zimeanza kuchukuliwa na wizara za kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata eneo la kufanyia shughuli zao ilikuepusha maafa.
Aliwataka kuacha kuvamia maeneo ya serikali hasa yale ya hatari ilikuepusha vifo visivyokuwa vya lazima kwa wakati huo.
Bashe alisema endapo wachimbaji hao wataendelea kuvamia maeneo ya serikali hatosita kuishawishi serikali kufungia lessein walizopewa haraka ilimaeneo hayo yabaki wazi kama hawato elewa.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO