Shirika la Ndege la Uturuki limezindua safari zake za moja kwa moja kutoka Instabul- Uturuki hadi Zanzibar. Safari hiyo ambayo ni kutoka Istanbul – Kilimanjaro – Zanzibar – Istanbul (IST-JRO-ZNZ-IST ) itakuwa ni mara tatu kwa wiki. Kuzinduliwa kwa safari hiyo kunafanya shirika hilo kuwa na maeneo 50 inayoyahudumia katika bara la Afrika. Kutokana na kuanzisha kwa huduma hiyo, shirika hilo ambalo linaheshimika duniani kutokana na kuwa na maeneo mengi inayotoa huduma za usafiri wa anga, litakuwa sasa lina maeneo 293 duniani ambayo inahudumia. Maeneo ya Afrika ambayo shirika hilo linatoa huduma zake ni pamoja na miji ya Afrika Mashariki ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, na Zanzibar; Nairobi, Mogadishu, Djibouti, Asmara, Addis Ababa, Kigali na Entebbe. img_3898

Ndege ya shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines), Boeing 737-900 ikiwa na abiria 150 ikipokea saluti ya maji wakati ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuanza safari tatu katika wiki za moja kwa moja kati ya Instabul na Zanzibar.

Ikiwa ni mruko TK567, ndege ya shirika hilo litawezesha wateja wake kuwa na safari ya moja kwa moja hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Istanbul wa Atatürk ambako kutoka hapo wataweza kuunganishwa na mji mingine muhimu ya Ulaya kama Frankfurt, Muscat, Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, Bombay, Copenhagen, Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, na Prague. "Shirika la ndege la Uturuki liko katika biashara ya kuhamisha elimu, mawazo, ndoto na fursa katika maeneo mbalimbali duniani. Tuko hapa leo kujenga daraja jingine kati ya dunia na Zanzibar, daraja ambalo pia litaimarisha uhusiano uliopo kati ya wananchi wa Uturuki na wa hapa Zanzibar", alisema Bw. Ahmet Olmustur, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Masoko wa Shirika la Ndege la Uturuki. Akifafanua zaidi kauli hiyo alisema: "Ni jambo la furaha kuona kwamba uzinduzi wa safari ya kuja Zanzibar na kwenda Instabul umefanyika kabla ya msimu wa sikukuu. Kutokana na hali hiyo, uzinduzi huu sio tu wa kuanzisha safari za ndege , bali ni sehemu ya maadhimisho ya hatua kubwa iliyopiga Zanzibar, Tanzania na Afrika kwa ujumla katika usafiri wa anga. Kupitia uwanja wa ndege wa Instabul, tutawaunganisha wasafiri kutoka Zanzibar kwenda katika vituo zaidi ya 161 duniani, kazi tunayoifanya kwa ufanisi kuliko shirika jingine lolote lile la ndege". eh4a8337 Kwa mujibu wa taarifa za Shirika hilo Tanzania inakuwa nchi ya 50 barani Afrika kufikiwa na Shirika la Ndege la Uturuki baada ya kuongezwa safari hizo tatu kwa wiki kwenda Zanzibar Hivi sasa shirika hilo lilikuwa linafanya safari 49 barani Afrika baada ya hivi karibuni pia kuongeza safari ya kwenda Visiwa vya Shelisheli. Likiwa ni shirika la nne kwa kuwa na mtandao mkubwa wa safari duniani kote kuliko mashirika mengine, ndege ya Shirika iliondoka Istanbul saa 6:30 usiku na kuwasili saa 3:30 asubuhi. Akizungumza katika tukio hilo la kihistoria, Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Balozi Ali Abeid Amani Karume alisema Zanzibar imefurahishwa sana kufanyakazi na moja ya mashirika ya ndege yenye mafanikio makubwa duniani ambayo yamekuwa yakitengeneza faida. eh4a8355

Ofisa Masoko Mkuu wa Shirika la ndege la Uturuki, Bw. Ahmet Olmustur (kulia) na Mjumbe wa bodi ya Shirika la ndege la Uturuki Ogun Sanlier wakishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar.

“Sisi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, tunakaribisha sana ushirikiano huu kwa sababu nyingi, kwa kuwa si tu inafungua lango la watalii lakini pia tunatengeneza fursa mpya kwa wananchi wetu”, alisema Balozi Karume. Pia aliamini kwamba kuja kwa ndege za Shirika hilo kutawezesha watu wengi zaidi kuja Zanzibar kwa utalii na pia kutoa fursa kwa watu mbalimbali wanaoanzia safari zao Zanzibar kuunganisha safari zao kwenda nchi mbalimbali Ulaya kwa urahisi zaidi. Aliwahimiza wananchi wa Zanzibar kutumia fursa hiyo kutengeneza nafasi ya nyingi zaidi za kibiashara na kuongeza idadi ya watalii nchini humo. Ndege ya shirika hilo la Uturuki aina ya Boeing 737-900 ikiwa na abiria 150 iliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume majira ya saa 3.30 asubuhi na kupokea saluti ya maji kabla abiria hawajaruhusiwa kushuka. Baadae ndege hiyo TK567 iliondoka Zanzibar saa 4:25 asubuhi na ilitarajiwa kuwasili Istanbul saa 11:45 jioni.

img_3958

Ofisa Masoko Mkuu wa Shirika la ndege la Uturuki, Bw. Ahmet Olmustur na Mjumbe wa bodi ya Shirika la ndege la Uturuki Ogun Sanlier pamoja na wageni walioshuka na ndege ya Uturuki wakiangalia burudani ya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar.

eh4a8395

Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mustafa Aboud Jumbe (katikati) pamoja na uongozi wa Shirika la ndege la Uturuki wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa safari hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar.

eh4a8411

Ofisa Masoko Mkuu wa Shirika la ndege la Uturuki, Bw. Ahmet Olmustur na Mjumbe wa bodi ya Shirika la ndege la Uturuki, Ogun Sanlier wakimshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mustafa Aboud Jumbe (wa nne kushoto) baada ya kuzindua rasmi safari hiyo.

eh4a8444

Mgeni rasmi Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Balozi Abeid Amani Karume (wa sita kulia) katika picha ya pamoja na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp (wa tisa kulia) pamoja na uongozi wa Shirika la Ndege la Uturuki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar.

eh4a8420

Ofisa Masoko Mkuu wa Shirika la ndege la Uturuki, Bw. Ahmet Olmustur (kushoto) na msafara wake wakielekea kwenye chumba maalum cha mapumziko baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar.

img_4016

Sehemu ya abiria waliotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar na Shirika la Ndege la Uturuki ikiwa ni safari ya kwanza visiwani humo.

img_4029

eh4a8509

Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Balozi Abeid Amani Karume akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hotel ya Park Hyatt visiwani Zanzibar. Kushoto ni Ofisa Masoko Mkuu wa Shirika la ndege la Uturuki, Bw. Ahmet Olmustur.

dsc_1069

Ofisa Masoko Mkuu wa Shirika la ndege la Uturuki, Bw. Ahmet Olmustur akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu safari mpya kutoka Zanzibar -Kilimanjaro-Istanbul (ZNZ-JRO-IST-ZNZ ) ambayo itakuwa ni mara tatu kwa wiki.

dsc_1119

Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua matukio muhimu yaliyojiri kwenye mkutano huo.

dsc_1058

Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp (wa pili kushoto) akichukua matukio ya picha katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa safari mpya ya Shirika la Ndege la Uturuki mjini Zanzibar.

eh4a8528

Ofisa Masoko Mkuu wa Shirika la ndege la Uturuki, Bw. Ahmet Olmustur (wa pili kushoto) akikabidhi mfano wa sanamu ya ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki Boeing 737-900 iliyopewa jina la Zanzibar kwa Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mh. Balozi Abeid Amani Karume kuashiria mwanzo wa mahusiano ya mawasiliano ya anga kati ya Uturuki na Zanzibar. Shirika hilo jana lilizindua safari za moja kwa moja kati ya Zanzibar na Instabul, Uturuki. Wengine wanaoshuhudia ni Mjumbe wa bodi ya Shirika la ndege la Uturuki Ogun Sanlier (wa pili kulia) na wafanyakazi katika ndege iliyotua jana mjini Zanzibar.

eh4a8527

Ofisa Masoko Mkuu wa Shirika la ndege la Uturuki, Bw. Ahmet Olmustur akimuonyesha jina la Zanzibar kwenye mfano wa sanamu ya ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki Boeing 737-900 Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mh. Balozi Abeid Amani Karume (kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika katika Hoteli ya Park Hyatt visiwani Zanzibar. Wa pili kushoto ni Mjumbe wa bodi ya Shirika la ndege la Uturuki, Ogun Sanlier.

eh4a8535

Mgeni rasmi Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mh. Balozi Abeid Amani Karume akiwa ameshikilia sanamu la ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki katika picha ya pamoja na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp (katikati), Ofisa Masoko Mkuu wa Shirika la ndege la Uturuki, Bw. Ahmet Olmustur (wa pili kushoto), Mjumbe wa bodi ya Shirika la ndege la Uturuki, Ogun Sanlier (wa pili kulia) pamoja na wafanyakazi katika ndege iliyotua jana mjini Zanzibar.

eh4a8543

Sanamu la ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki Boeing 737-900 iliyopewa jina la Zanzibar iliyotua jana mjini Zanzibar.

eh4a8549

Mgeni rasmi Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mh. Balozi Abeid Amani Karume na Mjumbe wa bodi ya Shirika la ndege la Uturuki, Ogun Sanlier wakiweka vituo Istanbul-Zanzibar kwenye ramani wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini Zanzibar.

eh4a8551

Mgeni rasmi Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mh. Balozi Abeid Amani Karume na Mjumbe wa bodi ya Shirika la ndege la Uturuki, Ogun Sanlier wakionyesha vituo vya safari ya Istanbul - Zanzibar kwenye ramani mbele ya waandishi wa habari.

eh4a8555

Picha ya pamoja baada ya mkutano na waandishi wa habari.

eh4a8557

Taarifa zaidi kuhusu ratiba ya safari:
Namba ya ndege Kuanzia Siku Kuondoka Kuwasili
TK 567 14 Desemba 2016 Jumatatu Jumatano Jumamosi Istanbul 20:30   3:20 (+1) Kilimanjaro
TK567 15 Desemba 2016 Jumanne Alhamis Jumapili Kilimanjaro 04:15 5:30 Zanzibar
TK 567 15 Desemba 2016 Jumanne, Alhamis Jumapili Zanzibar 06:25 13:45 Istanbul
    Muda uliotajwa ni wa LMT.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO