Ndege zikiwa uwanjani
WATU wapatao 20 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya ndege ya mizigo ya Uturuki (Turkish Airlines) kuanguka huko Kyrgyzstan.
Wengi wa waliouawa katika ajali hiyo ni wapita njia.
Ndege hiyo aina ya Boeing 747 ilianguka karibu na makazi ya watu karibu na uwanja wa ndege wa Manas  kiasi cha kilomita 25 kaskazini mwa mji mkuu wa Bishkek.
Vyombo vya habari vya hapa vimesema kuwa kuna idadi kubwa ya watoto waliokufa katika ajali hiyo.
Imeelezwa kuwa ndege hiyo ilikuwa inatoka Hong Kong ikitarajiwa kutua Manas kabla ya kuelekea  Istanbul, Uturuki.
Aidha imedaiwa kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya hapa ya  saa moja na nusu sawa na 01:30 GMT.
Ingawa uwezo wa kuona ulikuwa mdogo kutokana na  ukungu sababu ya ajali hiyo bado kuelezwa.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO