Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mfano wa Boarding Pass kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mahandisi Edwin Ngonyani kabla ya kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka   uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere,  Dar es salaam kwenda Dodoma Januari  16, 2017.  Alikuwa akizindua safari za ndege za shirika hilo kati ya viwanja viwili hivyo.

NDEGE mpya ya aina ya Bombardier Q400  jana ilianza safari za Dodoma
huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisema Serikali itaendelea kuboresha
Shirika la Ndege (ATCL) ili liweze kutoa huduma bora na kwa bei nafuu.
Kutokana na kuanza kwa safari hizo, sasa kutakuwa na ratiba ya mara
mbili kwa wiki kutoka Dar es Salaam, kupitia Dodoma hadi Kigoma.
Waziri Mkuu alisema  hilo ni tukio la kihistoria na mwendelezo wa
uboreshaji wa makao makuu ya nchi.
Alisema njia ya ndege itaendelea kuboreshwa mara wananchi walio karibu
na Uwanja wa Ndege watapolipwa fidia ili kuwezesha ndege kubwa zaidi
ziweze kutua.
“Tunafungua fursa zaidi na kuipa hadhi Dodoma kama makao makuu ya nchi” alisema
 Pia alisema  moja ya ahadi aliyotoa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, John Magufuli wakati wa kampeni ni kuboresha ATCL ili kutoa
huduma bora na kwa bei nafuu ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM).
Alisema nauli ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni Sh. 180,000 ikiwa
ni bei nafuu kulinganisha na mashirika mengine.
Pia alisema Juni mwaka huu serikali italeta ndege nyingine kubwaambayo
itaongeza ubora wa usafirishaji wa ndege hapa nchini.
“Watumishi wa serikali, wafanyabiashara watumie ndege zetu serikali
inahakikisha huduma zitakuwa bora na nzuri” alisema
Aidha aliwataka ATCL kujipanga kwa ajili ya kuboresha huduma ili
matumaini ya wananchi wa Dodoma yawe ya kweli.
Alisema Dodoma bado kuna nafasi ya kujengwa uwanja wa kimataifa eneo la Msalato.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister
Mhagama alisema serikali ya awamu ya tano inadhihirisha na kutekeleza
yote iliyoahidi watanzania na kila jambo waliloahidiwa litatekelezwa.
“Ndege zitanunuliwa na kwenda maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania” alisema
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela alisema serikali imefanya jambo
kubwa kuboresha usafiri wa kisasa mkoani Dodoma
Alisema serikali ielewe watu wa Dodoma wanafurahia sana kuanza kwa
safari za ndege za ATCL.
Spika wa bunge, Job Ndogai alisema jambo hilo limeandika historia mpya
katika mkoa wa Dodoma kwani kutakuwa na usafiri wa kisasa na wa
haraka..

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kabla ya kupanda ndege ya Shirika hilo kwenye uwanja wa Ngege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma  ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo,  Januari  16, 2017.

“Juhudi hizi ni kuimarisha Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na wana
Dodoma watumie fursa hiyo vizuri.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Faustin
Kamuzora alisema matengenezo makubwa yalifanyika katika uwanja wa
ndege Dodoma kwa ajili ya kuwezesha ndege kubwa kutua.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema tangu Rais afanye
maamuzi ya serikali kuhamia Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa alikuwa
kiongozi wa kwanza kuhamia Dodoma na uamuzi wa kuleta ndege Dodoma ni
kitendo cha ujasiri.
Alisema jambo hilo linafanya linaiweka nchi katika mazingira ya
yatakayosaidia kukuza biashara ya utalii kwa ujumla.
Mhandis Emmanuel Korosso ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya
Ndege  Tanzania alisema ahadi ya Rais kufufua ATCL imetekelezeka
ambapo Juni mwaka huu watapata itapatikana ndege nyingine ambayo
itasaidia kupanua wigo.
Alisema mwaka ujao watapata ndege nyingine itakayofanya kazi zake
masafa ya kati nay a mbali.
Alisema ndege hiyo itafanya safari zake siku ya Jumatatu na Ujumaa na
siku za safari zinaweza kubadilika siki za mbele kulingana na
mahitaji.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO