Usiku wa 31,December 2016 kuamkia mwaka mpya 2017 ndipo wanamitindo mbalimbali walikutana na kusherekea kwa pamoja Usiku wa Khanga yaani “Khanga Party”. Tukio hili kama lilivyo kuwa limetaarifiwa awali limefanyika Regency  Park Hotel.  Design mbalimbali za vazi la Khanga kutoka kwa wanamitindo zilioneshwa kwenye stage na kuzikonga mioyo za wadau pamoja na wahudhuriaji  usiku huo.

Kumbuka Party hii imeandaliwa na Mama wa Mtindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin, mbali na burudani zilizo kuwepo pia kulikuwa na Red Carpet yenye sifa kubwa ya kuwakutanisha mastaa na mashabiki wao kuweza kupiga picha za pamoja kwa ajili ya kumbukumbu. Tunawatakia mwendelezo mwema na wenye baraka wadau na wanamitindo kutoka hapa Tanzania. (Cheers 2017)Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO