Watu watano akiwemo mwanamke mmoja wamekamatwa na vichwa vinne vya biandamu ambavyo vinaonekana ni vya mauaji ya karibuni.
Watu hao wamekamtwa katika mpaka wa Ebonyi na Enugu  nchini Nigeria.
Polisi walikamata watu hao wakati wa ukaguzi wa kawaida wa basi majira ya saa nne asubuhi.
Tukio hilo la Fabruari 8 liliwaacha vionywa wazi wananchi wengine waliokuwa  ndani ya basi hilo la abiria.
Kwa mujibu wa Vanguard, lililokuwepo katika eneo la tukio watuhumiwa hao inaaminika walitoka Enugu wakielekea Cross River kupitia mpaka wa Ebonyi.
Imeelezwa kuwa maofisa usalama walilazimika kuwapiga risasi za miguu watuhumiwa hao walipojaribu kukimbia baada ya kubainika kwamba mizigo yao ilikuwa na vichwa vya binadamu.
Inaaminika maofisa usalama waliowatia mbaronbi watu hao ni kutoka Idarasa ya usalama wa ndani (DSS) kwani walikuwa wamevaa majaketi ya kuzuia risasi yaliyoandikwa DSS.

Imeelezwa kuwa watu hao baadae walichukuliwa na kupelekwa eneo lisilojulikana.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO