Rais Magufuli akitoa maagizo kwa Dc Maggid Mwanga

“Kuanzia leo (jana) isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi mwenyewe.”
Rais Joh Magufuli amesema hayo wakati akimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Majid Mwanga kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha Fukayosi wilayani humo.
Akaongeza, “Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na viongozi mlishughulikie hili kabla mimi sijawashughulikia nyinyi, wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Rais Magufuli aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam alitoa agizo hilo jana aliposimama katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi wengi wakiwa wamekusanyika kando ya Ofisi ya Kata.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji 

Baada ya kusimamisha msafara wake, aliwaita wananchi waliokuwa wamekusanyika huku wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka wafugaji wa jamii ya Wamang’ati waondolewe kisha akatoa nafasi kwa baadhi yao kueleza dukuduku lao.


Mmoja wa wananchi hao aliyejitokeza alisema wafugaji wa jamii za Wamang’ati wamekuwa wakiingiza mifugo katika mashamba ya mazao yao na wanapojaribu kuwakatza, wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.
Katika majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa kuwashambulia wananchi kwa viboko wakamatwe, Rais Magufuli alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima kuwapiga wafugaji.
Kadhalika, alimtaka kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifugo wao katika mashamba ya wakulima.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO