SHULE za shule za sekondari 178 katika mkoa wa Dodoma zimepatiwa
msaada wa mitambo ya umeme jua wenye thamani ya Sh. Milioni 218
na Shirika Lisilo la Kiserikali  la Zola linalojishughulisha na
usambazaji wa nishati ya umeme jua iliyopo nchini Marekani.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwenye shule ya sekondari ya
Ntyuka Manispaa ya Dodoma, Ofisa Mauzo Mkuu wa Shirika hilo lenye
makao yake mkoani Arusha, Ahmed Ndossa alisema lengo ni kuhakikisha
kiwango cha elimu kinapanda na kuongeza ufaulu wa wanafunzi mashuleni.
Pia ni njia ya kuwapatia hamasa wanafunzi wafanye vizuri katika masomo
yao na pia kuwekeza kimaendeleo kwenye serikali katika nyanja ya
kielimu.
Alisema mbali ya mitambo ya umeme huo wa jua pia vifaa vingine ambavyo
vimetolewa na shirika hilo na kufungiwa kwenye madarasa na maofisi ni
pamoja na televisheni, radio,chaja za simu tochi na taa.
Aidha alisema kufungwa kwa vifaa hivyo vya umeme katika shule hizo za
sekondari kutasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufikia malengo yao
kielimu kwani wataweza kujisomea wakati wote tofauti na hapo awali
ambapo walikuwa wakijisomea kwa kutumia koroboi na
mishumaa.
“Shirika la Zola lilibaini idadi kubwa ya wanafunzi mashuleni
wanashindwa kufikia malengo yao kielimu kama ilivyotarajiwa” alisema
Alitaja changamoto nyingine ni kuwa na muda mfupi wa kujisomea wakati
wa usiku sababu ya ukosefu wa umeme wa jua hali ambayo pia imechangia
kushindwa hata na mazoezi wanayopewa darasani kama vile miradina kazi
za nyumbani ambazo zingeweza kuchangia maarifa zaidi.

Alisema kuwa mradi huo umejiwekea malengo ya kuzifikia wilaya 23
Tanzania kwa mikoa ya kaskazini ambapo shule 171 kati ya 755 hazikuwa
na huduma ya umeme wa nishati yoyote mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu
kampuni hiyo itahakikisha wanafungiwa mitambo na Zola.
Ofisa Elimu sekondari mkoa wa Dodoma Leonard Ndossa alisema kuwa
mpango wa umeme jua ambao unawekwa na shirika hilo unaisaidia serikali
katika kuboresha elimu kwa wanafunzi ambao hawana nishati hiyo muhimu.

Alisema kuwa shule zilizo nyingi mkoa wa Dodoma hazina huduma wa
nishati ya umeme,hivyo kwa shirika hilo la Zola litakuwa limesaidia
kwa kiasi kikubwa kufanya vizuri masomo kwa kuwa watakuwa wana muda
mwingi wa kujisomea madarasami.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi,wazazi na walimu kuhakikisha wanakuwa
walinzi wa miundombinu ya umeme huo ili uweze kudumu na uweze kuleta
matunda ya kuleta maendeleo kwa wanafunzi.
Source:
Sifa Lubasi,

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO