UMOJA wa Afrika (AU) umempongeza Dk Tedros Adhanom kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kutoka ukanda wa Afrika.
Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa kamisheni ya AU, mheshimiwa  Moussa Faki Mahamat.
Katika pongezi zake alisema: “Dunia imeamua kumcgaua mtu ambays amebobea katika masuala ya afya ya jamii na usalama wa afya kama msingi wa maendeleo ya binadamu.”
Dk Adhanom aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro kigumu kilichowakutanisha Dk Sania Nishtar kutoka Pakistan na  Dk David Nabarro kutoka Uingereza.
Hivi karibuni Dk Adhanom alikuwa anashikiri kuandika rasimu ya agenda ya Umoja wa Afrika 2063(The African Union Agenda 2063) inayotengeneza mikakati ya maendeleo ya Afrika kwa kipindi cha miaka hamsini ijayo,akiwa mwenyekiti wa baraza tendaji la AU. 
Mheshimiwa Mahamat katika salamu zake amemtakia Dk Tedros mafanikio makubwa katika kazi yake hiyo mpya huku akisema kwamba AU itamuunga mkono katika haja za Dk Tedros zikiwemo za mabadiliko makubwa WHO ; afya kwa wote; uhakika wa afya; afya ya wanawake, watoto na vijana; mabadiliko ya tabia nchi yanavyoahiri masuala ya afya.
Mwenyekiti huyo amewashukuru mawaziri wa afya bara la Afrika kwa kuwa na msimamo wa pamoja katika kampeni na kusema kwamba bara hili linapokuwa pamoja linashinda.
Imesambazwa na APO kwa niaba ya kamisheni ya Afrika (AUC).


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO