Am sorry kwa hii post yangu ikimuumiza mtu, inahusu zaidi wale waigizaji wanaoitwa wenye sura mbaya au sura mbovu mbovu, miili isiyo na mvuto and wana vipaji ila wanalazimisha sana movies zao kucheza wenyewe uhusika ukuu movie after movie. nimeona films 4 a couple of weeks za wasanii hawa wa kibongo lakini sidhani kuwa ziliuza vizuri ingawa story zao nzuri. nililikuwa na jamaa flani na demu wake akawa anamcheka huyo muigizaji mkuu ambaye alicheza kama lover boy/playboy anayepapatikiwa na kinadada.
Nilielezea kwa kirefu hili months ago kuwa, commercial actors au mainstream actors iwe Hollywood au Bollywood hata katika hizo series za kikorea wanatakiwa wawe na talents na good looks, sexy appeal au mvuto , ni muhimu sana wanavutia mashabiki kibiashara. mnaokataa siwalazimishi.
But mara nyingi wenye sura mbaya inakuwa rahisi kucheza hata realistic films, art house films hizi zinahitaji sana talents mvuto wa mtu sio lazima sana kwasababu mara nyingi kuingiza mkwanja mkubwa sio lengo la films hizi lengo huwa kufikisha ujumbe zaidi, wanachezeshwa hata wasio mvuto na umaarufu wowote.
Sasa wenzangu na mimi sura ndio zile, miili nayo unakuta mtu mwembamba kama ufito au bonge kama bajaji unataka kucheza kila movie yako kama lead halafu sokoni uuze sana kama wenzio wenye mvuto au wanaojijali kimazoezi na misosi !
sokoni watu wanaangalia pia mvuto binafsi like I said kwa Hemedy it is important kwasababu hata movies alizocheza ni commercial by nature but hizi realistic and art house films Hemedy hakumfai huko as i said hata kipaji chake hakishawishi yeye kupewa movies za aina hiyo
Sasa inakuwa vizuri angalau mtu utengeneze mwili wako kwa mazoezi uvutie kwasababu kwenye TV kazi yako pia ni kuuza sura, si mnawaona kama kina The Rock au Dwaine Johnson hawa mvuto wa kuzaliwa ni zero, but mazoezi wameona na pengine kushauriwa ni muhimu sana ni. Commercial mbaya mbaya kufanikiwa kukaa kwenye game muda mrefu ni vigumu sana yaani huwa bahati sana kwa mmoja mmoja ndio sababu asilimia kubwa Hollywodd au India na hata hao Korea wote wana muonekano mzuri.
Hiki ni kitu kinachotiliwa maanani sana na casting directors wa commercial, mainstream newcomers watakaosumbua kwenye game baadaye.
Example diamond hana muonekano mzuri kiasili but ameji-update sana na kuwa kisasa, na pamba za maana, sasa hivi kila demu anamtaka Diamond, but ukimuangalia Diamond wa kamwambie, Mbagala na Kidogo, Nana, Salome ni vitu viwili tofauti ni kwasababu alijitambua mapema, kuwa serious na alichotaka kufanikiwa
I wanted to say kiwanda cha film na kiwanda cha muziki vinaitwa showbiz au show business yaani kiwanda cha kuuzia sura na show off huku biashara za film na muziki zikifanyika seriously kwa tafsiri isiyo rasmi. Yaani showbiz tuseme inahusu talent, performances, business na kuuza sura yaani show off nyingi example ni katika majarida na shoots nying.
So hata kama sura na muonekano wako havieleweki eleweki na unataka kuwa msanii ingia gym, fanya mazoezi, kula misosi ya kueleweka mwili vizuri, vaa kistaa off screen, as onscreen it depends on na character.
sababu kubwa wasanii wenye mvuto au muonekano mzuri huwa rahisi kucheza dark, grey character kubadilisha mionekano yao na kucheza characters za kisharobaro at the same time. pia kuvutia mashabiki sokoni ni point nyingine, kwenye world of endorsements, fashion world, magazine covers ndio wanahitajika zaidi, ndio hapo tunapata glamour world,
Na hata wale wasanii mlio na mvuto bado mazoezi ni muhimu sana, inawafanya muwe flexible na rahisi kucheza roles hata zile ngumu zinazotaka energy kubwa. sio mtu anacheza action movie dakika mbili tu anahema kama kafumaniwa, anataka maji ya kunywa na kupumzika kidogo, dakika mbili tena kadondoka kwa pressure.
Huo mvuto wa muigizaji niliosema ndio maana wanakuwa katika endorsements nyingi na shoots za hatari hatari au seductive kwenye shoots hasa za magazines ambazo zinamsaidia msanii husika kuingiza mkwanja but kama una sura mbaya utasubiri kuwa supporting zaidi , hujijali, ukipaka mafuta sura bado imepauka nani atakupa endorsements au magazine cover !
Source: Trim SaleemPost a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO