Jaji Kiongozi wa Tanzania Ferdinand Wambari (wa pili kushoto) akikagua kikosi cha askari wa kutuliza ghasia mkoa Kigoma muda mfupi baada ya kuwasili mkoani Kigoma kuanza ziara ya siku mbili kukagua shughuli mbalimbali za idara ya mahakama mkoani humo.(Picha na Fadhili Abdallah)

IDARA ya mahakama nchini imesema kuwa pamoja na maboresho makubwa yanayofanywa na idara hiyo katika kuongeza ujuzi wa wataalam wake,vitendea kazi na marupu rupu kwa watumishi wake mpango wa mahakama hiyo ni kuhakikisha inakwenda kwa wananchi na wananchi na kuwa kimbilio la wananchi katika kutafuta haki zao.

Jaji Kiongozi wa Tanzania,Ferdinand Wambari alisema hayo mjini Kigoma katika futari iliyoandaliwa na idara ya mahakama ya mkoa ambapo amesema kuwa ni lazima mahakama itimize wajibu wake katika kutoa haki kwa jamii na haki hiyo ionekane imetendeka.

Jaji Wambari ambaye yupo  kwenye ziara ya siku mbili ya kukagua shughuli za utendaji wa mahakama mkoani Kigoma alisema kuwa katika hilo ametaka wananchi waamini kuwa haki yao inapatikana mahakamani na kwamba kama Kiongozi Mwandamizi wa idara ya mahakama atahakikisha haki hiyo inapatikana tena inapatikana kwa wakati.

Pamoja na hilo alisema kuwa idara ya mahakama katika ngazi zote za mahakama inalazimika kuhakikisha kesho na mashauri mbalimbali yaliyopo mahakama yanashughulikiwa na kutolewa maamuzi katika kipindi kifupi ili kuondoa malalamiko ya muda mrefu ya wananchi kuhusiana na ucheleweshaji wa kesi uliokuwepo.

Awali Shekhe wa Mkoa Kigoma,Hassan Kiburwa msingi mkubwa wa amani ni upatikanaji wa haki na hivyo idara ya mahakama kwa ngazi zake zote za mahakama ihakikishe inatenda haki katika kutoa hukumu za kesi zinazofikishwa mahakamani.


Shekhe Kiburwa alisema kuwa anaridhishwa na mabadiliko ya utendaji na maboresho makubwa yanayofanywa kwenye idara ya mahakama jambo ambalo linatoa mwanga kwa wananchi kwamba mahala salama ambapo wanaweza kupata haki yao na kwa wakati ni mahakamani.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO