WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameongoza maelfu ya wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro katika maziko ya mbunge mstaafu wa jimbo la Moshi mjini, Philemon Ndesamburo(82) aliyezikwa nyumbani kwake mtaa wa KDC, kata ya Kiborloni Manispaa ya Moshi.
Mwanasiasa huyo na mfanybiashara mkongwe  alifariki ghafla Mei 31, mwaka huu wakati
akiwa ofisini kwake.
Viongozi wengine waliokuwepo ni pamoja na mwenyekiti wa taifa wa Chadema , Freeman Mbowe, mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
Wengine ni mwenyekiti wa CHAUMA, Hashim Rungwe, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Kilimanjaro, Vick Nsilo Swai,kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo,Zito Kabwe, John Shibuda, mwenyekiti wa IPP,Reginald Mengi.
Akiongoza ibada ya mazishi,katika kanisa Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Kiboriloni,  Mkuu wa Kanisa hilo,  Askofu Fredrick Shoo, alitaka waumini na watanzania kwa ujumla kujifunza na
kusimamia katika kutetea haki za wanyonge na makundi mengine ya kijamii.
Aliwataka viongozi wamuenzi Ndesamburo kwa kuacha ubinafsi.
"Ubinafsi  umekithiri naunadidimiza nchi yetu..., wewe Mungu amekupa nafasi kwa neema tu, umesomeshwa kwa fedha ya watanzania, watanzania  wamekupa nafasi uliyo nayo, halafu badala ya kuwatetea na kuwasaidia, ili waondokane na umaskini unakubali kupokea rushwa ili kupotosha haki ya wanyonge"
 Alisema ni viongozi wachache sana wanaotetea haki za wanyonge na wale wanaojitoa kwa dhati wanapigwa vita sana lakini aliwatia moyo na kuwataka waendelee kutenda mema na kutetea wanyonge.
Ndesamburo kwa ufupi
Alizaliwa Februari, 1935 katika kijiji cha Mahoma akiwa mtoto wa nne kati ya watoto wanane kwenye familia ya Mzee Ndesamburo Kiwelu, alifunga  ndoa 1962 na Ndehorio Ndemasi na kujaliwa watoto 12, wajukuu 26 na vitukuu tatu.
Mwaka 1944 hadi 1949 alisoma shule ya msingi Matemboni, Moshi, 1950-1953 alipata cheti cha kufuzu elimu ya msingi wa kati katika shule ya pili ya serikali Old Moshi.
1961 alipata cheti cha uhasibu katika Chuo cha Uhasibu cha Serikali, 1968-1969 alisoma katika Chuo cha Taaluma cha Thurack Uingereza na kupata diploma ya juu ya biashara ya kusafirisha mizigo kwa meli, na cheti cha juu cha bima ya mizigo.
Desemba 2016, alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima kutoka Chuo cha Biblia cha Japan, Mei 2016 alichaguliwa kuwa patroni wa One Accord Internation yenye makao makuu Lagos Nigeria, Mei mwaka huu alitunukiwa tuzo ya utumishi uliotukuka na World Evangelical Mission.
Ndesamburo alifanya serikali 1955-1960 alikuwa katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Serikali, 1961-1965 mhasibu Wizara ya Fedha, 1965-71 alifanya katika Wizara ya Mawasiliano na Wakala wa Kazi , 1971-72 alikuwa Mkurugenzi Mtendaji akihusika na kupakua na kupakia mizigo bandarini mizigo yote ya serikali, 1972-75 alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ujenzi na Barabara.
Aidha  alikuwa anajihusisha na biashara mbalimbali zikiwemo za usafirishaji, kupakia na kupakua mizigo bandarini, hoteli na utalii wa ndani na nje ya nchi.
Alianza siasa tangu wakati wa harakati za uhuru wa Tanganyika, 1988 alikuwa mmoja wa watanzania walioanzisha madai ya vyama vingi vya siasa na kuundwa kwa Umoja wa Demokrasia (UDETA), mwaka 1992 Sheria ya Vyama Vingi ilipitishwa rasmi, pia alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Chadema akiwa na kadi namba 10.
Alikuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa miaka 15 kuanzia 2000-2015, mwakaa 2006-10 alipata nafasi ya kuwa Kamishna wa Bunge pia kwa nyakati tofauti alikuwa mjumbe wa kamati mbalimbali bungeni ikiwemo Kamati  ya Hesabu za Serikali, Biashara na Viwanda, Waziri kivuli wa Wizara ya Maliasili.Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO