Saudi Arabia ambayo ina dhamana ya ulinzi katika maeneo matatifu ya miji ya Meca na Madina imesema imefanikiwa kutibua shambulio la mhanga lililokuwa lifanyike katika msikiti mkuu wa  Mecca.
Imeelezwa na watu wa usalama wa Saudia kwamba  mhanga huyo alijifumua mwenyewe katika nyumba aliyiokuwamo baada ya kubaini kwamba amezingirwa na maofisa usalama.
Imeelezwa kuwa jingo hilo lilibomoka na watu 11 kujeruhiwa wakiwemo askari polisi.
Aidha watuhumiwa wengine watano wamekamatwa.
Mamilioni ya Waislamu wamekusanyika mjini Mecca kwa ajili ya kuadhimisha kuisha kwa mfungo  wa Ramadhani.
Mamlaka  za Saudi Arabia hakuwatoa habari zaidi.
Katika miaka ya karibuni Saudi Arabia imekuwa ikikabiliwa na wimbi kubwa la mashambulio ya mhanga yanayodaiwa kupangwa na kutekelezwa na kundi la Islamic State.
Mengi ya mashambulio hayo yamekuwa yakifanywa dhidi ya wafuasi wa Shia na maofisa usalama wa taifa hilo.

Julai 2016, maofisa usalama wanne  waliuawa katika shambulio la mhanga lilililofanyika karibu na msiki wa Mtume mjini Medina.

Saudi Arabia ni moja ya nchi zilizoungana kukabuiliana na  wapiganaji wa IS na makundi ya Jihadi nchini Syria na Iraq.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO