Tamko la THBUB wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16, 2017

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote wa haki za watoto duniani katika kuadhimisha “Siku y...





Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote wa haki za watoto duniani katika kuadhimisha “Siku ya mtoto wa Afrika”. Siku hii inaikumbusha dunia juu ya mauaji ya watoto wapatao 2,000 wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini, waliouawa kikatili miaka 41 iliyopita na iliyokuwa Serikali ya Makaburu.

Siku hii ilizinduliwa rasmi mwaka 1991 na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ili kuwakumbuka watoto hao waliokuwa wakidai haki ya kutobaguliwa na haki nyingine za binadamu.

Wakati tunaadhimisha siku hii muhimu wadau wote wa haki za watoto hatuna budi kujitathimini namna tunavyowaandaa watoto wetu ili waweze kutoa mchango stahiki katika maendeleo ya taifa letu, kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu inayosema: “Maendeleo endelevu 2030: Imarisha ulinzi na fursa kwa watoto wote.”

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizochukua hatua mbalimbali kuhakikisha uwepo wa maslahi ya watoto. Hatua hizo ni pamoja na kutunga sheria na kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda inayolinda na kutetea haki za mtoto. Mikataba hiyo inajumuisha: Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto (1989), Tamko la Shirika la Kazi Duniani (ILO) Na. 182, na Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (2003).

Miongoni mwa sheria zilizotungwa katika ngazi ya kitaifa ni: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), Sheria ya Mtoto Na. 21/2009, Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sheria  ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA (1998).

Pia imeridhia na kubuni sera, mipango na mikakati mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo: Sera ya Mtoto (2008), na Mpango-kazi wa Kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017- 2022).

Kimataifa imeridhia na inatekeleza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDG’s) yaliyopitishwa mwaka 2015 yanayobainisha kuwa watoto wana haki ya kuishi, kulindwa, kutobaguliwa na kushirikishwa kwa usawa ili kuhakikisha kuwa wanapata fursa sawa katika jamii.

Ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kinara wa kujali haki za watoto Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia imeanzisha taasisi na vyombo mbalimbali vinavyoshughulikia ulinzi na ukuzaji wa haki za watoto nchini. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni miongoni mwa taasisi hizo.

Tume imekuwa ikitoa elimu ya haki za binadamu, ikiwemo haki za watoto kupitia vyombo vya habari, semina na mikutano  mashuleni na maeneo mbalimbali inayopata fursa ya kuyafikia.

Pia, Tume imekuwa ikitoa huduma za kisheria kwa makundi yenye uhitaji ambao ni pamoja na watoto na watu wengine wenye uhitaji wa msaada wa kisheria na pia imeanzisha dawati mahsusi linaloshughulikia haki za watoto.

Vilevile, Tume imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali wa haki za binadamu kimataifa na kitaifa ili kuweka nguvu ya pamoja katika kulinda haki za binadamu na kukemea vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi yao.

Aidha, kupitia Mpango-kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu (National Human Rights Action Plan - 2013-2017) Tume imefanikiwa kutoa mafunzo kwa waalimu na watendaji wengine katika sekta ya elimu na kuhamasisha uanzishwaji wa vilabu takriban 130 vya haki za binadamu shuleni. Pamoja na mambo mengine vilabu hivi vinajihusisha na utoaji wa elimu ya haki za binadamu ikiwemo elimu ya haki za watoto, shuleni na nje ya shule.

Juhudi hizo ni muhimu kipindi hiki katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia azma yake ya “Kujenga Tanzania ya Viwanda.”

Pamoja na jitihada hizi zote bado zipo changamoto mbalimbali zinazoathiri malezi ya watoto na kuwanyima fursa katika jamii, changamoto hizo ni pamoja na: umaskini, migogoro ya wanandoa, mila potofu, utandawazi, majukumu ya kijinsia katika jamii na ukosefu wa haki ya elimu ya afya ya uzazi (reproductive and health rights).
Tume inaitaka jamii kuwapa umuhimu watoto wa kike na kuachana na mtazamo potofu kuwa hawana mchango mkubwa kwa jamii, hali inayochangia utumikishwaji wa watoto na kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na biashara ya ngono katika umri mdogo.

Vitendo hivyo vimekuwa chanzo cha mimba na ndoa za utotoni ambazo huwaletea madhara mbalimbali ikiwemo: unyanyasaji wa kimwili, kisaikolojia, kingono, athari za kiafya, vifo wakati wa ujauzito/kujifungua na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU).

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) mwaka 2014, tatizo la ndoa za utotoni lipo duniani kote. Takriban wasichana milioni 15 wanaolewa kila mwaka chini ya umri wa miaka 18. Ikiwa ni wastani wa watoto wa kike 41,000 kwa siku.

Utafiti huo ulibaini kuwa tatizo la mimba za utotoni kwa Tanzania ni kubwa, ambapo wasichana 4 kati ya 10 (sawa na asilimia 40) wanaolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

Pia kwa mujibu wa takwimu za demografia ya afya Tanzania (TDHS, 2016) asilimia 36 ya wanawake wa kitanzania wenye umri wa miaka kati ya 20-24 waliolewa au waliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa mara ya kwanza kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.

Takwimu zilizotolewa na Shirika la Watoto Duniani (UNICEF, 2012) zimeitaja Mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni kuwa ni: Mkoa wa Shinyanga ukiongoza kwa asilimia 59. Ikifuatiwa na Tabora (58%), Mara (55%), Dodoma (51%) na Lindi (48%).

Hivyo basi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapendekeza na kutoa wito kama ifuatavyo:
1.     Serikali ifanye marekebisho ya sheria kandamizi na zinazopingana na sheria zingine. Mfano;- Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inaweka miaka 18 kuwa umri mdogo ambao wavulana wanaruhusiwa kuoa, lakini imeweka umri wa miaka 15 kwa wasichana kuolewa kwa ridhaa ya wazazi.

2.     Mamlaka zinazotoa haki kwa wahanga wa ukatili, wakiwemo watoto zitoe haki kwa wakati.

3.     Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ihakikishe uwepo wa mfumo utakaowawezesha watoto wa kike wanaopata mimba mashuleni kuendelea na masomo yao mara tu wanapojifungua.

4.     Wadau wa haki za binadamu waendelee kutoa elimu ya haki za binadamu kwa jamii, ili kubadili mila na tamaduni potofu. Pia kukemea vitendo vya ukatili, unyanyasaji na udhalilishaji wa watoto.

5.     Wazazi wawajibike katika malezi ya watoto ili kuimarisha familia zao na kuwaepusha na viashiria hatarishi kwa maisha ya watoto wao.

6.     Watoto wapatiwe elimu ya afya ya uzazi ili waweze kujitambua na kuwa na uelewa juu ya madhara ya mimba na ndoa za utotoni.

7.     Wadau mbalimbali wa haki za watoto kuhakikisha kuwa ulinzi, usalama na haki za mtoto vinaimarishwa. Aidha, wahakikishe watoto wa kike na wa kiume wanapatiwa malezi bora yanayotoa fursa sawa kwa wote ili kuhakikisha kuwa ndoto zao katika maisha zinafikiwa.

8.     Wadau wote wa haki za binadamu kuhakikisha kuwa kama taifa tunaondoa aina zote za ukatili na ubaguzi dhidi ya watoto na kuwapa haki na fursa sawa katika umiliki wa rasilimali na nyanja zote za kimaisha na kusimamia Sheria na Sera zinazolinda usawa wa kijinsia ili taifa letu liweze kufanikisha lengo la fursa sawa kwa wote ifikapo mwaka 2030.

Imetolewa na:
(SIGNED)

Salma Ali Hassan
(Kamishna)

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Juni 16, 2017

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Tamko la THBUB wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16, 2017
Tamko la THBUB wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16, 2017
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjKCi3GaOmEC2gf9oxM0Uo4pvyfMyNcq7MQNT_lV5Dy2Qwut0Ux8qYxeZIt461WNS2QefECLwWdbW8jHA4BP5kF0jfCugyFghLyt5UtgVD4vRQFiSA1hCYRDQEYSfFizUv6GuzDuPAhvGw/s320/haki.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjKCi3GaOmEC2gf9oxM0Uo4pvyfMyNcq7MQNT_lV5Dy2Qwut0Ux8qYxeZIt461WNS2QefECLwWdbW8jHA4BP5kF0jfCugyFghLyt5UtgVD4vRQFiSA1hCYRDQEYSfFizUv6GuzDuPAhvGw/s72-c/haki.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2017/06/tamko-la-thbub-wakati-wa-maadhimisho-ya.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2017/06/tamko-la-thbub-wakati-wa-maadhimisho-ya.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy