NI miaka 30 tangu Stanley Kubrick atengeneze kitu hiki kinachoitwa Full Metal Jacket, picha ambayo inazungumza kizaazaa cha vita nchini Vietnam.

Nimeamua kuzungumza hivi kwa kuwa Juni 17 mwaka huu, sinema hii imetimiza miaka 30 tangu kuachiwa kwa wapenzi wa sinema.

Ni moja ya sinema ambazo walio wengi wanaikumbuka hasa kwa aksheni zake na hasa yule mkufunzi ambaye alionekana kuwa balaa.

Inaanza vyema hasa yale mafunzo ya Marine (askari wa Marekani ndivyo wanavyoitwa) tayari kwa vita nchini Vietnam. Na kw ajinsi sinema uilivyo ni kama vile Marine ni askari hatari wanaoringia uaskari wao na mafunzo yao, lakini ukiangalia filamu hii unaona pia ubinadamu wao.

ndani ya sinema hii kuna watu walilazmika kula san akuonekana wanene na wasiogaa katika Marimne na  huyu alipata taabu sana kwani yeye kimsingi utamuona kama ndiye hasa dango la kisaikolojia la kijeshi katika kmumfanya mtu kuwa mkakamavu na kupunguza woga.


Na katika hili pia kuna watu walikuwa wakimkosea kwa makusudi ili aweze kutoka katika ile platuni inayofunzwa kuwa ndio staa wa vita.

Mafunzo  hayo yaliyokuwa yanaendeshwa na sajini balaa — Hartman —  na huyu ndiye anayeamua kwamba mtu yule mnene Pyle ni lazima ale mzigo na atoke katika platuni anayoifunza, anaudhi.


Stanley Kubrick iameipanga vyema sinema hii kuonesha ukali wa mafunzo na pia tabia mbaya za askari katika vita tabia ambazo zinaonesha ubaya wa vita na wkamba vita haiwezi kuwa na kioo chema kwa jamii.

“Full Metal Jacket,” imetengeneza wauaji na kuonesha ni kwa namna gani watu wa kawaida wanaklazimishwa kuwa wauaji wakatili kabisa. Kiukweli sinema hii ambayo imeandikwa pia nae akisaidiana na mtu mwingine ni sinema ambayo si rahisi sana kuiangalia, lakini toka ukianza hadi unamaliza,kemikali katika mwili wako zinakuwa juu bila kushuka.
Kama nilivyosema awali sinema hii imetengenezwa wakati majadiliano ya kilichojiri Vietnam kikiwa ndio ajenda ya wamarekani na wasanii wa filamu.
Hata hivyo Kubrick, ambaye alifanya sinema nyingi zenye ukakasi mkubwa wa utata  katima kichwa cya waonaji sinema wengi kama :'A Clockwork Orange,' 'Lolita,' 'Dr. Strangelove,' na  '2001: A Space Odyssey' ameileta sinema hii tiofauti ndio maana kuitazama pamoja ya kwamba yataka moyo lakini toka unaianza mpaka unamaliza, huna raha kama wewe ni mtu wa kawaida.
Hakika hii ni filamu ya undava undava na huna neno la karibu la kuelezea fiolamu ambayo kwa kiingereza nasema kusema ni mean and cruel. Filamu hii inakufanya usijisikie vizuri hata chembe.
Ingawa sinema hii imegawanyika pande mbili kuu, yaani mafunzo na vita yenyewe haina maneno sana zaidi ya aksheni. Huwezi kujua kipande hadi kipande lakini unaweza kujiuliza swali kama nilivtyosema hapo juu hawa watu wa kawaida wameandaliwa kufanya nini hasa kuua? Unaona kwa sababu Pyle pamoja na kubanwa na kuwa mtu wa kupigiw amfano alipata mfadhaiko wa akili akamuua Hartman na pia kujiua. Kwa maneno mengine hapa  unaweza kuchanganya kujua nia ya mtengeneza sinema. Hakupenda namna watu walivyotengenezwa kuwa wauaji.

Kubrick anaua mtu mmoja hadi mwingine na mwishoni vitani kule mdunguaji ambaye alikuwa binti mdogo aliyesumbua kwelikweli jeshi la Marekani anaonekana na anaomba auawe na anayeua anaopat dhiki kubwa lakini anaua kisha  Kubrick anatuonesha kitu kumbe katika vita furaha ni kuw amzima na kuondoa woga.. Yaani pamoja na sinema hii kuiona miaka 30 iliyopita  hakika nakumbia  hell No shit!

Imetoka awali habarileo Jumapili

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO