Beyonce na mumewe Jay Z wameipa dunia majina ya watoto wao mapacha waliozaliwa hivi karibuni.
 Majina yao ni  Rumi na Sir Carter!
Kwa mujibu wa habari zilizofikishwa Us Weekly  zinasema kwamba ni kweli watoto hao wamepewa majina hayo kama ilivyoripotiwa na TMZ kwa mara ya kwanza.
Mapcha hao wa kiume na kike walizaliwa Juni 12 ikiwa ni miaka mitano baada ya  binti yao anayeenda kwa jina la Blue Ivy.
Mapacha hao wamezaliwa Ronald Reagan UCLA Medical Center,  huko Los Angeles ambapo Queen Bey na mumewe walikodi ghorofa nzima (floor) ili kutengeneza faragha ya kutosha ya mke kujifungua.
Majina yametolewa wakati pia rapa Jay-Z ametoa albamu mpya 4:44 ambapo misitari aliyochana inaonesha kufunguka kwake kuomba radhi kwa Beyonce kwa  kutokuwa mwaminifu.
“I apologize often womanize / Took for my child to be born / See through a woman’s eyes / Took for these natural twins to believe in miracles / Took me too long for this song / I don’t deserve you,” hayo ndiyo maneno utakayosikia katika wimbo huo uliobeba albamu .

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO