KWA mara ya kwanza katika historia ya Tamasha la filamu la kimataifa la Zanzibar, maarufu kama tamasha la nchi za jahazi, (ZIFF) litatoa tuzo pamoja na fedha kiasi cha dola 14,000 kwa ujumla wake.
Aidha kumekuwepo na tuzo zaidi na tamasha la mwaka huu ambalo ni la 20 litafunguliwa na sinema kutoka  nchini, T junction.
Aidha soko Filam litajumuisha na  watu wa Discop na hivyo tamasha la mwaka huu kuonesha mabadiliko makubwa katika uendeshaji na fursa zinazotokana na kuwapo kwake.
Tamasha hilo litakaloanza Julai 8 hadi 16 pia litakuwa na  mbio za ngalawa mara mbili zitakazofanyika Nungwi na Mji Mkongwe kwa siku tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari na wadau katika mkutano wa mwisho wa utambuzi wa kitakachojiri katika tamasha hilo kubwa Afrika Mashariki na Kati, Mtendaji mkuu Fabrizio Colombo alisema kwamba fedha hizo zitasaidia kupunguza gharama za watengenezaji na pia kutoa nafasi ya kutengenezwa kwa filamu nyingine.
Katika tuzo hizo, tuzo ya Sembene itakuwa na  jumla ya dola za Marekani 6,000 wakati mtawanyiko mwingine ni kati ya dola 1000 na 2,000 huku tuzo ya jahazi la dhahabu, tuzo kuu ya ZIFF itaambatana na dola 3,000 zitakazotolewa na Showmax. Aidha  mwanamke atakayetengeneza dokumentari bora ataondoka na dola za Marekani 2,000.
 Katika mkutano huo wa uzinduzi wa tamasha  la ZIFF, juzi ambapo ratiba ya mwisho ilitamngazwa rasmi na wadhamini, ilielezwa kuwa sinema  zipatazo 20 za Tanzania ziliingia katika tamasha mwaka huu lakini tano tu ndio zina ubora wa kimataifa.
 Miongoni mwa sinema hizo ni Kiumeni, Stolen Soul, Hofu, Usiku wa Kiza na Seed  of Momeries.
 Ikisherehea miaka 20 na uongozi mpya wa fabrizo Colombo aliyeanza kazi Novemba mwaka jana baada ya Profesa Martin Mhando kumaliza muda wake na kuomba asiendelee, itaonesha filamu zaidi ya 150 katika kipindi cha takribani siku 7, kuendesha makongamano na kufanya maonesho mbalimbali ya sanaa.
 Wakidhaminiwa na  ZanLink, ComNet , Azam Marine, GIZ, Double Tree Hilton na Ethiopian Airlines, tamasha litakuwa na wageni zaidi ya 100 kwa ajili ya soko Filam pekee litakalofanyika Park Hyatt Julai 12-14.Washiriki hao pia watakuwa katika majadiliano ya biashara na madaraja maalumu ya elimu kuhusu utengenezaji wa sinema.
 Patna wengine katika tamasha la mwaka huu ni Ubalozi wa Marekani, Milele Zanzibar Foundation, taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Italia ijulikanayo kama The Foundation ACRA.

Wapo pia Trace Mziki, ambao wanadhamini  tuzo ya muziki ya ZIFF inayotolewa kwa mara ya kwanza(ZIFF East African Music Video), CloudsTV, African Film Channel, Omenka magazine, DarLife, na Zanzibar24 ..

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO