BAADA ya miaka saba ya kubebwa, watengeneza sinema wa Bongo, watatakiwa kujitegemea katika kushiriki tamasha lijalo la kimataifa la filamu za Zanzibar, ZIFF.
Tamasha hilo ambalo pamoja na kuonesha filamu  zikiwemo zilizo katika mashindano, pia hutoa nafasi ya elimu ya utengenezaji wa sinema, uandishi wa sinema utoaji sauti katika sinema na umuhimu wa muziki katika sinema.
Mwaka huu kuna mtawanyiko wa mafunzo kuanzia utayarishaji wa sinema mpaka mauzo kukiwa na soko la  mauzo ya sinema kwa ajili ya televisheni na majumba ya sinema.
Kauli ya ZIFF iliyotolewa na Ofisa Mtendaji wake Daniel Nyalusi imetokana na swali aliloulizwa na mmoja wa waigizaji, projuza, mwandishi wa filamu na muimbaji Irene Sanga.
Katika swali lake pamoja na ushauri alitaka kujua kama kampuni kubwa zinazotengeneza sinema nchini pamoja na waigizaji wenye majina walialikwa katika hafla ya utambuzi wa kinachokuja katika ZIFF. Alisema kukiwa na malalamiko ya masoko na ubora wa kukatisha tama ilikuwa vyema kama wahusika na tasnia hiyo wangelikuwepo.
Aidha alitaka kujua kama ni halali kuendelea na watu ambao hawataki kutumia fursa wanazopewa kuinua tasnia na kuwaacha chipukizi ambao wako tayari kujifunza na kuinyanyua tasnia ya filamu.
Alisema kwa miaka yote amehuhudia watu wenye majina makubwa nchini katika sanaa ya uigizaji wakipewa ‘vya bure’ kuhudhuria tamasha hilo, huku kwenye maeneo muhumu kama hayo ambayo wanapaswa kuwepo kwa ajili ya kutengeneza uhusiano na kujuana hawafiki.

Nyalusi alisema kwamba  amealika watu wote wakiwemo wenye majina lakini kinachomshangaza yeye  ni hata hiyo jana (juzi) kwenye hafla iliyofanyika jumba la utamaduni la balozi wa Ujerumani  hawakufika huku mwingine pamoja na kuwa na kadi anamuuliza hafla hiyo inafanyika zanzibar au Dare s salaam.
Alisema kwa miaka saba amejaribu kuwapatia fursa nyingi za kujifunza ili kunyanyua tasnia ya sinema nchini, lakini wale wanaooonekana kujua wameacha  kuhudhuria na kuomba nafasi mbalimbali ambazo majirani wakenya wanazitumia.
Katika hafla ya utambulisho wa kazi zitakaooneshwa katika tamasha la 20 la ZIFF huko Zanzibar,  Nyalusi alikiri kwamba watanzania wengi hawatumii nafasi na Fursa zilizopo  ZIFF ikiwamo ya masoko na elimu ili kubadili filamu kuwa katika soko la kimataifa lenye ushindani wa filamu.
Katika kuchangia hoja ya Irene, Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mahmoud Thabiti Komb amesema kwamba  watanzania tuna matatizo mengi ya kutotumia fursa ambazo zipo mbele yetu.
Alisema wamealika wasanii wote na  cha maana walipaswa kukumbatia jukwaa linalowapa nafasi ya kukutan ana wengine kwa lengo kuongez amtandao na pia kufanikisha mauzo ya kazi au kuziboresha zaidi.
Alimtafadhalisha Irene kuwapatia orodha ya chipukizi ambaow ako tayari kujifunza kwa kuwa wao lengo lao ni kuhakikisha kwamba tasnia inakua na Tanzania inangia katika  ramani ya filamu bora.

Tamasha la Filamu mwaka huu linafanyika likiwa na mabadiliko makubwa ikiwamo shindano la shule za filamu ambapo Kenya na Afrika Kusini wameingiza wanafunzi wao huku Tanzania ikishindwa kupeleka .

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO