MENGI AIPA TWCC JENGO LAKE KUENDELEZA UJASIRIAMALI

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD, amekipatia Chama cha ...

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD, amekipatia Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania ( TWCC) jengo la maonyesho la IPP Ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali. Jengo hilo pamoja na kuendeleza ujasiriamali litakuwa eneo la maonesho na kufunzia na Dk Mengi amesema amelitoa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwawezesha wanawake kiuchumi. Maamuzi ya kutoa jengo hilo yalifuatana na ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa TWCC Jacqueline Maleko aliyetaka jengo hilo kupewa wanawake ili kuwaendeleza kiuchumi na kimafunzo. Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce-TWCC), Dk Mengi aliwataka wanawake kuwa macho na kutumia fursa zilizopo kujiwezesha kiuchumi. [caption id="attachment_3593" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mwakilishi wa TRA, Rose Mahendeke (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini TWCC, Bi. Noreen Mawalla (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini (TWCC), Bi. Jaqueline Mneney Maleko (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.[/caption] Aliwataka wanawake kuthubutu na kuwa wajasiri katika kuangalia na kuzitumia fursa zilizopo sasa nchini badala ya kuzipita bila kuziona. Aidha Dk Mengi aliwataka wanawake wajiamini na kujihakikishia kwamba wanaweza kujiletea maendeleo, wawe wanyenyekevu katika biashara zao, na wawe na ndoto kubwa ya maendeleo huku wakianza kidogo kidogo badala ya kusubiri mtaji mkubwa. Katrika mkutano huo Dk Mengi alitoa ushuhuda wa jinsi yeye alivyoanza biashara zake na kusema alitumia fursa alizoziona kutengeneza dawa ya kung’arisha viatu baada ya kuchukua mkaa Kariakoo na kuusaga na kuchanganya na mafuta. Alisema alitengeneza dawa iliyoitwa ‘Sunshine’ na alivuna mapesa. [caption id="attachment_3597" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.[/caption] Aidha alisema kwamba alianzia kutengeneza kalamu ndani ya sebule kabla hajaondoka na kutumia maeneo ya nje kutengeneza kalamu na kasha kuwa na kiwanda kikubwa. Alisema yeye alizaliwa katika umaskini akiishi katika nyumba ya msonge pamoja na wanyama na kuamua kuukataa umaskini. Alisema kilichomsaidia yeye ni kuwa na macho yanayoona Fursa na kuitumia vilivyo kwa kujiamini na kuthubutu. Alisema Mungu aliumba kila mtu kuwa namba Moja na ni vyema watu wote wakajiona kuwa namba moja na katika hilo kuthubutu huku wakihakikisha kwamba wanatumia vyema teknolojia iliyopo kwa kufanya matangazo ya biashara zao. [caption id="attachment_3594" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania TWCC, Bi. Noreen Mawalla akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania TWCC Jacqueline Meney Maleko (hayupo pichani) kutoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wanachama wa TWCC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa TWCC uliofunguliwa jana jijini Dar es Salaam.[/caption] Aliwataka kutumia simu zao kuhakikisha kwamba wanauza na kuzitangaza bidhaa zao huku akiwataka wakue na kuacha kuogopa kuanzisha viwanda. Pia aliwataka kuwa wanyenyekevu katika biashara zao kwani ndio namna bora ya kuendeleza urafiki wa kibiashara kati yao na wadau wanaohitaji huduma au bidhaa zao. Alisisitiza utoaji wa bidhaa bora hata kama bidhaa hizo zimelenga kuwasaidia watu maskini na kuwataka kila senti wanayoipata katika biashara kuhakikisha inabaki hukohuko na isichanganywe na matumizi binafsi. Mapema akimkaribisha mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Mwenyekiti TWCC, Jacquiline Maleko alipendekeza Chama chake kiwe na ushirikiano na uwakilishi mkubwa kwenye taasisi muhimu za biashara na kuyataka makampuni binafsi nchini yawe yananunua bidhaa za wanachama wao kabla ya kupendelea bidhaa za nje. [caption id="attachment_3595" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Dr. Reginald Mengi kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa TWCC unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.[/caption] Maleko pamoja na kumuomba Dk Mengi, kuipatia TWCC jengo lililopo Sabasaba pia aliitaka TPSF (sekta Binafsi) kuhakikisha kwamba inawazungumzia wanawake na kuwapa nafasi katika vikao vya maamuzi. Pia alifafanua kwamba chama hicho kinataka kushirikishwa katika baraza la biashara la kitaifa na mikoani kwa lengo la kutetea wanawake ambao asilimia 50 ya wafanyabiashara nchini ni wao. Maleko alisema chama hicho kilichoundwa mwaka 2005 na kwa sasa kikiwa na majukwaa 11 pote nchini, kimelenga kuunganisha nguvu za wanawake katika kuhakikisha wanashika uchumi kwa kutumia fursa zilizopo za nafasi mbalimbali za wanawake zilizowezeshwa kitaratibu, kama asilimia 5 ya mapato ya halamashauri kusaidia makundi maalumu na asilimia 30 ya zabuni ya manunuzi ya serikali kupewa makundi maalumu. [caption id="attachment_3596" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Louis Accaro akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es Salaam.[/caption] Alishauri asilimia hiyo tano kukopeshwa SACCOS yao wanawake ili waweze kukopa na kuendeshea biashara zao, akiamini kwamba fedha hizo zikifikishwa zitawatoa wanawake kiuchumi. Alisema kwa sasa wanawake wafanyabiashara wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya mila, desturi na taratibu za kisheria na hivyo wao ni kazi yao kuhakikisha kwamba sauti ya mwanamke inafika kila mahali ili mazingira ya biashara yaboreshwe. Maleko pia alisema kama serikali inaweza kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa kwanini na wao wasipewe ruzuku hiyo ili waweze kuinua uchumi wa taifa. Pia waliomba nafasi katika maeneo ya Taasisi ya viwanda vidogo SIDO kutumiwa na wanawake kuanzisha viwanda vya kusindika vyakula ambapo pia wanaweza kufundishwa na watalamuwa SIDO wakiwa palepale. [caption id="attachment_3599" align="aligncenter" width="1404"] Meneja mikopo ya wanawake na uwezeshaji wanawake wa benki ya CRDB nchini, Rehema Shambwe akitoa salamu za benki hiyo kwa wajumbe wa TWCC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.[/caption] Mkutano huo wa mwaka ulifadhiliwa na Mamlaka ya Kodi na Mapato TRA, uilikuwa na wageni wengi wakiwemo watu wa CRDB ambao wanampango wa kuanzisha kituo cha kusaidia wanawake katika masuala ya biashara na ujasiriamali na Trade Mark ambao tayari wanaushirikiano na TWCC. Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga alisema Asasi yake ipo katika hatua za mwisho za kuingia mkataba mpya wa miaka 5 wenye thamani ya shilingi bilioni mbili na Chama hicho, baada wa ule wa mwanzo wa shilingi milioni 650 kuhitimishwa. Mkataba huo wa mwanzo ulishughulika na mafunzo kwa wajasiriamali katika nyanza zote kuanzia uzalishaji na ufungashaji na matumizi ya hati mbalimbali zinazogusa ujasiriamali. [caption id="attachment_3600" align="aligncenter" width="1404"] Mwakilishi wa TRA ambao ndio wamefanikisha kufanyika kwa mkutano huo, Bi. Rose Mahendeke aktioa salamu za TRA kwa wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3601" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga akitangaza kuhusiana na hatua za mwisho za kuingia mkataba mpya wa miaka 5 wa thamani ya shilingi bilioni mbili na TWCC, baada wa ule wa mwanzo wa shilingi milioni 650 kuhitimishwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3602" align="aligncenter" width="6000"] Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko akishuhudia Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akiweka kwa maandishi kukabidhi jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga.[/caption] [caption id="attachment_3613" align="aligncenter" width="1404"] Picha juu na chini ni wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3603" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko (katikati) kibali cha jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wake kuendeleza ujasiriamali. Kulia Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga.[/caption] [caption id="attachment_3605" align="aligncenter" width="1404"] Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akisalimiana na wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3606" align="aligncenter" width="1404"] Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD katika picha ya pamoja na wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Saalaam.[/caption] [caption id="attachment_3608" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC, Bi. Noreen Mawalla.[/caption]

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MENGI AIPA TWCC JENGO LAKE KUENDELEZA UJASIRIAMALI
MENGI AIPA TWCC JENGO LAKE KUENDELEZA UJASIRIAMALI
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2018/01/DSC_5691.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2018/01/mengi-aipa-twcc-jengo-lake-kuendeleza.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2018/01/mengi-aipa-twcc-jengo-lake-kuendeleza.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy