JESHI  limefanikiwa kubaini  kiwanda cha silaha ambacho kimekuwa kikiwawezesha majambazi silaha za kufanyia uhalifu.
Habari zinasema kwamba kiwanda hicho kipo nyumbani kwa mhunzi kilikutwa kikiwa na  silaha mbalimbali zilizokuwa zikitengenezwa kienyeji.
Aidha askari wamefanikiwa kumtia mbaroni mwenye kiwanda hicho baada ya kumnasa muuzaji wa silaha wakati akienda kupeleka oda kwa jambazi.
Kiwanda hicho kwa mujibu wa taarifa kipo jimbo la Nasarawa, Nigeria.
Mtu huyo alikamatwa akiwa na silaha kielekea kuziuza kwa mkuu wa genge la kihalifu aliyetambulika kwa jina la  Damina Saminaka.Katika taarifa iliyosainiwa na Brigedia jenerali Sani Kukasheka Usman mnamo Januari 10 mtuhumiwa, Mohammed Bello, alidakwa akiwa na silaha barabara kuu ya Akwanga  iliyopo jimbo la Nasarawa.
Baada ya kubanwa mtuhumiwa alisema kwamba amenunua silaha hizo kutoka kwa mhunzi Dan Asabe Audu.
Ndipo askari hao walipoenda eneo hilo na kubaini kuwapo kwa kiwanda cha silaha na huku nyingine zikiwa zimekamilika zikisubiri wanunuzi.
Jeshi limesema kwamba watuhumiwa haow atakabidhiwa kwa mamlaka husika ili sheria ifuate mkondo wake.
Mtuhumiwa huyo alikuwa ndani ya gari aina ya  Opel Vectra ma alikuwa anaelelea Saminaka kukutana na kiongozi wa majambazi Damina Saminaka. Ilielezwa kuwa katika mahojiano silaha hizo alizokutwa nazo zilikuwa zimenunuliwa kwa naira elfu 30 (N30,000.00k).
Wamesema  askari kuwa Dan Asabe Audu, akikiri katika maohijiano kwamba alikuwa katika biashara hiyo kwa kipindi kirefu sasa.
Kiwanda hicho kilikuwa na zana zote zinazotakiw akutengeneza silaha katika hatua zake zote na pia walikuta silha katika hatua tofauti.
Katika ukaguzi huo wlaikuta silaha tatu ambazo rtayari zimekamilika,20 zikiwa katika hatua mbalimbali, uniti 7 za kasha tupu za risasi za mm9, risasi ya 9mm , mashine mbili za kutobolea genereta moja na simu tatu.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO