Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imewatia hatiani na kuwatupa jela miezi mitano Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘sugu’ na mwenzake Katibu wa Chadema Kanda, Emmanuel Masonga.

Hukumu hiyo ilitolewa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite.

Katika hukumu hiyo  iliyosomwa kwa takribani saa mbili kuanzia saa 3.30 asubuhi hadi majira ya saa 11:15 asubuhi alisema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kwamba ni kweli maneno hayo yalitamkwa na washitakiwa na kwamba maneno hayo yalimlenga Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO