Kutoka kwa Markus Mpangala
Ramani ya Jiji la Dar es Salaam mwaka 1957 kuonyesha mgawanyo wa mashamba na makazi. Maeneo mengi ambayo yameainishwa kama mashamba ya mpunga katika ramani hii, sasa yanatumika kama makazi, na hukumbwa na adha kubwa wakati wa mvua.
Ramani kwa hisani ya J. A. K. Leslie.
kUTOKA KWA BEDA
 Hakika kama tunataka kuendelea kuishi hapa ni lazima kufanya engeneering babu kubwa hii ramani kama ndio ukweli wenyewe tufa!

Mama Prof. Anna Tibaijuka anasema;
Bila nidhamu ya kuheshimu Mipango miji mafuriko yatakuwa common feature ya jiji la DSM. Regrettably. Tatizo siyo mvua kubwa. Tatizo ni kuziba natural drainage system hivyo maji ya mvua kushindwa kwenda baharini.
Nilipokuwa Ardhi nilijitahidi sana kuokoa bonde la msimbazi kwa mujibu ya 1979 master plan. Call it the Nyerere Master plan.
Sikufanikiwa. There was no political will for it. Bonde likaendelea kujengwa. Kwa hiyo maji hayana njia za kufika baharini.
Mind you Bonde la Msimbazi ndiyo njia pekee kwa maji yote yatokayo Pugu Hills Ukonga Airport Tazara Tabata Kigogo magomeni Ilala kufika Jangwani grounds hadi salender bridge yanapoingia baharini. Pia maji kutoka ubungo Manzese Tandale magomeni Kagera kinondoni hananasif Muhimbili hadi jangwani njia ni hiyo tu moja.
Kwa upande wa chuo kikuu mto mbezi na mto mlalakuwa na mto Mdumbwi ( Kawe) imejengwa na njia za maji kuifikia kuzibwa. You do not need to be an expert in urban planning to know that WATER FINDS ITS OWN LEVEL. ALSO TO KNOW THAT IN SOME YEARS HEAVY RAINS SHALL BE EXPERIENCED. ALL THESE THINGS ARE PREDICTABLE.
Mfano at Jangwani grounds Tulisema lakini uharaka wa kukamilisha mradi wa DART uka overide any other consideration. Nilisikitika sana knowing it was a recipe for disaster lakini urban planning is a political activity. Without the support of political power, all knowledge and expertise go to waste. They cannot help much.
Nimeona nielezee hili kwa watu wanaotaka kujua kwa nini wataalam wametufikisha hapa. Sio wataalam. No interests. Na utamaduni wa kutoheshinu utaalam. Na wananchi kutaja quick solutions. Going forward lazima kurejea plan ya Mwalimu ya 1979. To salvage the Msimbazi Valley as THE CENTRAL CITY PARK. Waliojenga wawe resettled with compensation kama wanastahili. New developments in this valley ziwe arrested.
Mama T in Dodoma Bungeni


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO