Wafanyabiashara ndogo ndogo wanaouza kando kando  ya barabara ya Mazimbu road kata ya kihonda mkoani Morogoro wametakiwa kuondoka katika eneo hilo na kuelekea eneo la soko.
Akizungumza na Lukwangule Afisa Mtendaji wa kata ya Kihonda Omary Jaba amesema kuwa wafanyabiasha hao wamekuwa wagumu kuondoka katika barabara hiyo  licha ya kuwaambia mara kadhaa waende kwenye maeneo husika yaliyotengwa kwa ajili ya soko. 
Alisema kuwa kata ya Kihonda inamaeneo ya soko matano na yote yametelekezwa licha ya kuwa matatu kati ya hayo yameshapimwa na wafanyabiashara walishaanza kujenga.
"tulishaongea na viongozi wao eneo walilopo sio sahihi na sio salama kutokana na kukaa karibu na barabara kuna mabodaboda ambayo yapo kisheriahivyo hata usalama wao na wateja wao ni mdogo, Alisema Jaba.
Aidha aliyataja maeneo matatu kati ya matano yaliyotengwa kwa ajili  ya masoko katika kata hiyo ambayo tayari yameshapimwa na kuanza kujengwa kuwa ni  mtaa wa Kilimanjaro,mtaa wa azimio na mtaa wa msimamo.Jaba alieleza kuwa serikali iliwataka wafanyabiashara hao kupitia viongozi wao wachague eneo moja la soko ili wakawagawie wafanye biashara badala yake wamekataa na kuendelea kuwepo hapo
Naye mfanyabiashara Asha Kibwana  ameiomba serikali iwaache wafanye biashara katika eneo hilo kutokana na wingi wa watu hasa nyakati za usiku hivyo  ufanyaji biashara kwao unakuwa rahisi.
"Rais alishasema tuachwe tufanye biashara kokote sasa kwa nini wao  watuambie tuende huko azimio wakati hapa ndio kwenye biashara,"alisema asha.
Issa Shabani mkazi wa Kihonda Manyuki alieleza kuwa ni vyema serikali ikawatafua eneo la karibu na hapo ili kuwasaidia wafanyabishara hao kuweza kuendesha maisha yao ya kila siku.
"hiki kama kituo cha kubadili gari wanaoenda lukobe, Manyuki, Yespa na maeneo mengine wengi kama hawajapanda ya moja kwa moja watashukia hapa wanaunganisha usafiri wakifika hapa watanunua tumahitaji yao  ya vyakula, hasa wanaotoka kazini usiku," alisema Issa 
Source: Na Maua Magona

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO