Arusha, Tanzania : 23 Aprili, 2018:

KUNDI la wataalamu wanaotekeleza mradi wa kimataifa wenye lengo la kuongeza uzalishaji wandizi kwa nchi za Uganda na Tanzania, wanakutana mjini Arusha wiki hii, kwa nia ya kutathmini maendeleo ya mradi huo na kupanga shughuli zinazotakiwa kufanyika mwakani.

Wataalamu hao wanaofanya utafiti wa migomba watakutana kuanzia tarehe 23 hadi 27 Aprili katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  (NM-AIST) iliyopo mjini Arusha.

Ndizi ni zao la chakula na pia chanzo kikuu cha mapato kwa mamilioni ya wakulima wadogo wa migomba katika nchi za i Tanzania na Uganda. Mataifa haya mawili ndiyo yanayozalisha nusu ya ndizi zinazozalishwa barani Afrika zenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 4.3 kila mwaka.

Hata hivyo wakulima hao kwa sasa wanazalisha asilimia 9 tu ya uwezo wao wa uzalishaji kutokana na athari za wadudu na magonjwa yanayokumba zao hilo.

Mradi huo wauzalishaji wa mbegu bora ya migomba umelenga kuwapelekea wakulima mbegu bora ya migomba yenye kuzaa zaidi na kukabiliana na magonjwa .

Mbegu hiyo inatarajiwa kuipita mbegu inayotumika sasa katika uzalishaji kwa zaidi ya asilimia 30 kwa mazingira yaleyale.

Mradi huo umejikita zaidi katika kufanikisha kuendelea kuwapo kwa aina mbili za mbegu ambazo ni maarufu kwa ukanda huo, Matooke na Mchare ambayo hulimwa sana nchini Tanzania.

“Mradi huu wa uzalishaji wa mbegu bora umejikita zaidi kuwapatia wakulima mbegu wanayoipenda na yenye kuhimili matatizo ya msingi ya sasa. Hata hivyo, ni vigumu sana kupata miche ya migomba aina inayotakiwa kutokana na zao hilo kutokuwa na mbegu au punje. Wazalishaji mbegu wanapata mbegu kwa kutumia mgomba wenyewe na mchakato wake huchukua muda mrefusana,” anasema Profesa RonySwennen, mzalishaji kiongozi wa migomba katika Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo katika kanda ya Tropiki (IITA) ambaye pia ni Mtafiti kiongozi wa mradi huo.

“Watafiti katika mradi huu wanafanya kazi pamoja kwa kutumia utaalamu wa kisasa zaidi katika maabara zetu duniani kote ilikukabiliana na changamoto za uzalishaji wa mbegu hizi, kuharakisha mchakato wake wauzalishaji na kuongeza uzazi wa aina mpya ya miche ya migomba yenye kuzaa zaidi na kuhimili magonjwa nawadudu,” alisema Profesa Rony Swennen.

Mradi huo unawaleta pamoja watafiti waandamizi wa migomba kutoka nchi za Australia, Ubelgiji, Brazil, Jamhuri ya Czech, India, Kenya, Malaysia, Afrika Kusini, Sweden, Tanzania, Uganda naMarekani.

Mradi huo ambao sasa uko katika mwaka wa tatu, umewezesha Tanzania kwa mara ya kwanza kuwa na programu ya kuzalisha migomba na mbegu ya kwanza ya ndizi Mchare iliyofanyiwa kazi kwak uunganishwa na migomba poriy enye uwezo mkubwa wa kuhimili magonjwa, umepandwa mwaka huu 2018. Uzalishaji wa mbegu za Matooke upo katika ngazi za juu na kwamba  zaidi ya miche 250 ya Matooke iliyofanyiwa utafiti imechaguliwa kufanyiwa  majaribio nchini Uganda na Tanzania.

Magonjwa ambayo yanatazamwa sana ni mnyauko na Sigatoka nyeusi ya migomba na upande wa wadudu ni minyoo (au kwa kitaalamu parasitic nematodes ) na wadudu wanaokula migomba ambao ni fukuzi (au kwa kitaalamu Weevils).

Uzalishaji huo wa mbegu bora unaenda sambamba na utafiti wa kuelewa ukubwa wa kiwango cha uharibifu na kusambaa kwa wadudu na magonjwa hayo na kutengeneza mfumo wa haraka wa kutambua magonjwa na kuzalisha mbegu ambazo zinahimili changamoto hizo.

Katika mradi huu imebainika pia kwamba ugonjwa wa Sigatoka unasambaa katika maeneo mengine na huenda ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ili mradi huo uwezekuwa endelevu,pia unawafunza watafiti wa baadae wa migomba kwa kuwapatia nyenzo mpya za ufundi na utaalamu wa kisasa wa uzalishaji wa mbegu bora za migomba.

Pia mradi unatoa nafasi ya kubadilishana  vinasaba vya migomba kati ya nchi na maabara tofauti kwa ajili ya utafiti na kutumia kinasaba bora kwa ajili ya kutengeneza mbegu mpya, ikianzisha ushirikiano wa kimataifa wa mfumo wa uzalishaji wa migomba duniani.

Mradi huo unaoongozwa na kuratibiwa na IITA kwa ushirikiano na wadao wengi nchini  Tanzania na Uganda.

Shughuli ya uzalishaji wa mbegu hiyo mpya ya migomba inafanyika katika Taasisi ya Sayansi naTeknolojia ya Nelson Mandela  (NM-AIST) Arusha, Tanzania kwa ushirikiano wa karibu na Taasisi za Utafiti wa Kilimo nchini Tanzania (ARI) katika maeneo yanayozali shandizi; na Programu ya uzalishaji wa migomba kwenye Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa kilimo ya Uganda (NARO) katika maabara za Kawanda na Sendusu, mjini Kampala.
Description: https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif

Mradi huu unaendeshwa kwa mujibu wa taratibu za utafiti za CGIAR za mazao ya mizizi na ndizi (RTB).

Kwa habari zaidi tembelea: http://breedingbetterbananas.org/


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO